• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

DED KITETO AWAPONGEZA WALIMU KWA KUPANDISHA UFAULU KIDATO CHA NNE

Imetumwa : February 1st, 2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, CPA. Hawa Abdul Hassan, amewapongeza kwa dhati walimu na watendaji wote wa sekta ya elimu wilayani hapa kwa jitihada, kujitoa na moyo wa uzalendo uliosaidia kuleta mabadiliko makubwa ya ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne 2025.


Akizungumza kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya mtihani huo uliofanyika Novemba 2025, CPA. Hawa amesema mafanikio hayo si ya bahati nasibu, bali ni matokeo ya kazi kubwa inayofanywa na walimu kwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau wa elimu, kwa lengo la kuhakikisha watoto wa Kiteto wanapata elimu bora na yenye ushindani.


“Nawapongeza sana Walimu wangu mahiri kwa jitihada kubwa kutufikisha hapa. Ninathamini sana jitihada zao na kujitoa kwao,” amesema CPA. Hawa.


Katika matokeo hayo, Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto imeongeza ufaulu kutoka asilimia 92.9 mwaka 2024 hadi asilimia 97.8 mwaka 2025, hatua inayothibitisha kupanda kwa kiwango cha taaluma na ufanisi wa mikakati iliyowekwa katika sekta ya elimu.


Akielezea sababu za mafanikio hayo, Mkuu wa Divisheni ya Sekondari wilayani Kiteto, Mwl. Ally Kichuri, amesema ongezeko hilo limetokana na juhudi za makusudi za Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu pamoja na kuimarisha rasilimali watu.


“Mbali na kuboresha miundombinu ya elimu, mafanikio haya yamepatikana baada ya serikali kuajiri walimu wapya, jambo lililopunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa walimu wilayani hapa,” amesema Mwl. Kichuri.


Kwa kuangalia mwenendo wa ufaulu kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, Kiteto imeonesha safari ya maendeleo yenye mwelekeo chanya na wa kudumu. Mwaka 2023 ufaulu ulikuwa asilimia 90.6, mwaka 2024 ukaongezeka hadi asilimia 92.9, huku mwaka 2025 ukifikia asilimia 97.8. Ongezeko hili linaonesha kuwa uwekezaji katika elimu, usimamizi thabiti na moyo wa kujitoa kwa walimu vinaendelea kuzaa matunda yanayoonekana wazi.


Kwa mafanikio haya, Kiteto haijaongeza tu asilimia za ufaulu, bali imeimarisha imani ya jamii kuwa elimu ni nyenzo muhimu ya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, huku walimu wakibaki kuwa nguzo kuu ya safari hiyo ya mafanikio.


Katika matokeo hayo, Mkoa wa Manyara u eshika nafasi ya pili kati ya mikoa 31 kitaifa, jambo ambalo linaupa mkoa heshima na hadhi katika sekta ya elimu nchini.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA MAPOKEZI YA FEDHA SEPTEMBA 2025 September 16, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU September 01, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • DED KITETO AWAPONGEZA WALIMU KWA KUPANDISHA UFAULU KIDATO CHA NNE

    February 01, 2026
  • KAMATI YA FEDHA YAKAGUA MIRADI YA BILIONI 1.4, YASISITIZA UWAJIBIKAJI

    January 31, 2026
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LAPITISHA BAJETI YA SHILINGI BILIONI 41.9 KWA MWAKA WA FEDHA 2026/2027

    January 27, 2026
  • DC MWEMA AAGIZA USIMAMIZI MADHUBUTI WA SHERIA NA ULINZI WA MIUNDOMBINU YA SERIKALI

    January 26, 2026
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa