Timu ya wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri, CPA. Hawa Abdul Hassan, Machi 28, 2025, wameutambulisha mradi wa mabweni mawili kwa Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Dosidosi.
Akiongea katika mkutano huo, Mkurugenzi huyo amesema kwamba Halmashauri imepokea kiasi cha TZS 260,000,000 kupitia mradi wa EPforR II kwaajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya wanafunzi wa Sekondari ya Dosidosi.
Vilevile, CPA. Hawa aliwaambiwa wajumbe wa kamati hiyo kua wana jukumu la kwenda kuutambulisha mradi huo kwa wananchi na kuwahamasisha juu ya ushiriki wao katika utekelezaji wa mradi huo ili mradi uweze kukamilika kwa wakati.
" Mradi huu ni wenu, nawaomba wananchi wote kusaidia kulinda vifaa vyote vitakavyo kua vinaletwa hapa kwaajili ya utekelezaji wa mradi huo", aliongeza CPA. Hawa.
Aidha Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Ndg. Godfrey Mwangairo, alitoa muongozo wa uundaji wa kamati mbili za utekelezaji wa mradi huo.
Mbali na hilo, ametoa wito kwa wajumbe hao kwenda kuwahamasisha wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi waliopo ndani ya kata hiyo kujisajiri kwenye Mfumo wa Kieletroniki wa Manunuzi ya Umma (NeST) ili waweze kuomba tenda za vifaa vya ujenzi wa mradi huo.
Nae Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Kiteto,Ndg.Venance Sangawe, amesema kwamba Taasisi yake itakua na jicho la karibu katika mradi huo ili kuhakikisha thamani ya mradi inaonekana.
Ukamilikaji wa mradi huu utawanufaisha wanafunzi 160 kwa kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shule na kuwapunguzia baadhi ya wazazi gharama za kuwapangishia wanafunzi vyumba eneo la karibu la shule. Aidha ukamilikaji wa mradi huu unatarajia kupunguza utoro na kuongeza ufaulu katika shule hiyo.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa