Januari 15, 2024, timu ya Maafisa Afya Mazingira ikiongozwa na Ndugu Bakari Hassan Soni, imefanikiwa kufika katika shule za msingi Chemchem, Kibaya,Kaloleni na Ngarenaro kwaajili ya kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa Kipindupindu na namna ya kuepukana na ugonjwa huo.
Miongoni mwa vitu walivyosisitiza maafisa hao ni ujenzi na matumizi ya vyoo bora, umuhimu wa wananchi kufanya usafi wa mazingira mara kwa mara ili kujikinga dhidi ya magonjwa ya kuhara na kutapika kama kipindupindu.
Mbali na elimu, timu hiyo imefanikiwa kugawa dawa za kutakasa maji ya kunywa (waterguard) kwa wanafunzi wa ahule hizo, kwaajili ya kwenda kutumia na familia zao.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa