Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Mwema Emmanuel, ameiagiza Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Wilayani Kiteto kuvitembelea vikundi vilivyonufaika na Mkopo wa 10% wa Halmashauri na kuendelea kuwapa elimu ya ujasiriamali vikundi hivyo ili kuwawezesha kutumia mikopo hiyo kwa nia waliyokusudia na kuweza kurejesha fedha hizo kwa wakati.
Mhe. Mwema ametoa maagizo hayo kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Mikopo ya 10% kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Walemavu iliyofanyika katika Kijiji cha Ndedo Machi 25,2025.
Aidha Mhe. Mwema amevisihi vikundi hivyo vilivyonufaika na Mkopo huo awamu ya sasa, kupambana ili kuweza kurejesha fedha kwa wakati kama ilivyokusudiwa ili vikundi vingine viweze kunufaika na mkopo huo.
Akitoa taarifa ya Mikopo iliyotolewa, Mratibu wa Mikopo ya 10% katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Ndg. Rufina Haule, amesema kwamba mpaka sasa Halmashauri imetoa mikopo yenye thamani ya TZS 389,125,000 kwa vikundi 103.
Mratibu huyo aliendelea kusema kwamba, katika fedha hizo, vikundi 49 vya wanawake wamenufaika kwa kupata mkopo wa TZS 164,000,000, vikundi 39 vya vijana vimepata TZS 163,000,000 na vikundi 15 vya walemavu vimepata mkopo wenye thamani ya TZS 62,125,000.
Sehemu ya fedha za mikopo zilitotolewa kwa vijana zimeweza kununua pikipiki 10 kwa vikundi vitano vya vijana huku upande wa walemavu, sehemu ya fedha hizo za mkopo zimenunua pikipiki za miguu mitatu (guta) tatu, kwaajili ya walemavu watatu kama walivyoomba.
Mhe. Mwema alitoa rai kwa wanufaika wa vyombo hivyo vya moto kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu zote ikiwemo kuvikatia vyombo hivyo bima.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa