• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

FAHAMU CHIMBUKO LA KAMPENI YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA DUNIANI.

Imetumwa : December 9th, 2023

FAHAMU CHIMBUKO LA  KAMPENI YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA  DUNIANI.

Kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10 Dunia hufanya kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia lengo likiwa ni  kupinga ukatili na kutetea haki za wanawake.

Ukatili wa kijinsia ni kitendo chochote ambacho anaweza kutendewa mwanaume, mwanamke au mtoto na kitendo hicho huweza kumuathiri kimwili au kisaikolojia. Wanawake na watoto ndio wamekua wahanga wakubwa wa kufanyiwa ukatili wa kijinsia.

Toka mwaka 1981, wanaharakati wa haki za wanawake wamekua wakiitumia Novemba 25, kuadhamisha kupinga ukatili ili kuwaenzi wanaharakati wa kisiasa watatu (Mirabal Sisters) ambao waliuwawa mwaka 1960 huko Jamhuri ya Dominika mwaka 1960, kwa amri ya aliyekua kiongozi wa nchi hiyo Rafael Trujillo.

Mwaka 1993 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake kwa kuweka mikakati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana..

Azimio hilo lilipelekea Baraza hilo mwaka 2000 kuweka azimio likitaja rasmi Novemba 25 kua ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya  Wanawake. Tamko hili lilipelekea serikali , pamoja na mashirika yasiyo  ya kiserikali na taasisi mbalimbali, kuunga nguvu za pamoja na kuandaa shughuli mbalimbali zenye lengo la kuufanya umma kuongeza ufahamu juu ya suala  la kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Mwaka 2006, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Awamu ya saba Ndugu Koffi Annan, alitaka Dunia itambue kua ukatili wa Kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wa kike limekua tatizo kubwa hivyo aliona kuna haja ya kua na kipindi maalumu cha kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia.  Hivyo ilikubalika kampeni hiyo ianze Novemba 25 ambayo ni Siku ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia na kuhitimishwa  Desemba 10 ambayo ni Siku ya Haki za Binadamu Duniani.

Lengo la kampeni hii ni kuongeza ushawishi, kubadilishana taarifa na uzoefu, kujenga uwezo wa pamoja, matumizi mazuri ya rasirimali zinazopatikana na kuunganisha nguvu za asasi za kijamii katika kuhamasisha, kuelimisha, kukemea na kuchukua hatua kwa pamoja ili kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii.

Hivyo basi Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia inalenga kupaza sauti ili kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu athari hasi za ukatili wa kijinsia na njia za kuondokana na unyanyasaji huo katika jamii.

Serikali pamoja na wadau mbalimbali wanaotetea Haki za Binadamu, hufanya shughuli mbalimbali katika kampeni hiyo ikiwemo midahalo mbalimbali ya hadhara au kwenye taasisi  kama vile shuleni na vyuoni.

Ofisi ya Ustawi wa Jamii Wilayani Kiteto ikishirikiana na Ofisi ya Maendeleo ya Jamii pamoja na taasisi isiyo ya kiserikali ya KKKT-USAID Kizazi Hodari (Kanda ya Kaskazini na Mashariki); imefanya maadhimisho hayo kwa kupita katika shule saba  na  kutoa elimu kuhusu kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi katika shule hizo walifundishwa aina za ukatili wa kijinsia ikiwepo ukatili wa kimwili, ukatili wa kihisia na ukatili wa kingono. Aidha wanafunzi hao walielezwa madhara ya ukatili wa kijinsia ikiwemo magonjwa, kupata mimba za utotoni, kuathirika kisaikolojia na kuharibika mwili. Mbali na hayo wanafunzi hao walidokezwa kuhusu viashiria vya ukatili wa kijinsia na kuwataka wanafunzi hao kua makini.

Pamoja na hayo, wanafunzi hao walielezwa sehemu sahihi za kutoa taarifa endapo watafanyiwa ukatili wa kijinsia au endapo watabaini mwenzao amefanyiwa ukatili wa kijinsia.

Mbali na elimu hiyo, taasisi ya KKKT-USAID Kizazi Hodari  ( Kanda ya Kaskazini Mashariki) ilitoa msaada wa madaftari kwa baadhi ya wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu.

Shule zilizotembelewa na maafisa hao ni pamoja na shule nne za shule za Msingi ambazo ni Kibaya, Chemchem, Kaloleni na Msente ilhali upande wa shule za sekondari ni Kibaya, Partimbo na Kiteto.

Kauli mbiu ya Kampeni hiyo kwa mwaka 2023 ni “WEKEZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA”.

Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPTEMBA 2023 September 03, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABIA MBAYA ZA WATUMUSHI ZINAHARIBU SIFA ZA TAASISI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LIMEMPONGEZA RAIS SAMIA.

    May 30, 2025
  • PONGEZI KWA WANANCHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

    April 28, 2025
  • TUUENZI MUUNGANO WETU

    April 27, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa