Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), CPA. Hawa Abdul Hassan, amewaasa wajumbe wa kamati hiyo kuhakikisha wanatenda haki katika kushughulikia masuala ya ukatili wilayani Kiteto.
Hayo aliyazungumza katika kikao kilichoketi Desemba 5, 2025 kujadili utekelezaji shughuli zilizotekelezwa na wajumbe wa kamati hiyo katika Robo ya Nne ya Mwaka 2024/25 na Robo ya Kwanza ya 2025/26.
Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho,CPA. Hawa aliwasisitiza wajumbe hao kuhakikisha kuwa kila mmoja wao ahakikishe anasimamia haki katika nafasi yake, ili wahanga wa ukatili wapate haki zao kwa wakati.
“Kila mmoja wenu akitimiza wajibu wake kwa haki, tutakuwa tumewasaidia wahanga kupata haki zao na pia tutakuwa tumepambana kutokomeza ukatili wilayani kwetu. Kila mmoja ajue majukumu haya amepewa na Mwenyezi Mungu msipotekeleza majukumu yenu ipasavyo, maana yake mnawanyima haki wahanga kwa kufanya hivyo mtakua na lakujibu mbele ya Mwenyezi Mungu,” alisisitiza CPA Hawa.
Aidha, CPA Hawa aliwataka wajumbe kuendelea kushirikiana kwa karibu, kuweka mbele maslahi ya wahanga na kuhakikisha taarifa zote za ukatili zinasimamiwa ipasavyo hadi hatua ya mwisho, ikiwemo kuhakikisha watoto na wanawake wanaopitia madhila wanapata faraja, ulinzi na msaada wa haraka.Katika kikao hicho, wadau walionesha hatua muhimu walizochukua kukabiliana na vitendo vya ukatili, zikiwemo kampeni za elimu, ufuatiliaji wa kesi, huduma kwa manusura na kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama wa watoto na wanawake.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa