Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mh. Lairumbe Mollel akizungumza na vijana baada ya uzinduzi wa SACCOS ya vijana uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamim Kambona akizungumza na vijana katika uzinduzi wa SACCOS ya vijana uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto.
Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii ndugu Joseph Mwaleba akitoa neno la ukaribisho kabla ya uzinduzi wa SACCOS ya vijana uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto.
Mkuu wa idara ya kilimo ,umwagiliaji na ushirika halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Robert Urassa akizungumza katika uzinduzi wa SACCOS ya vijana uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto.
Afisa ushirika ndugu Joseph Mwanga akitoa maelekezo kuhusu taratibu za uanzishwaji na uendeshaji wa SACCOS baada ya uzinduzi wa SACCOS ya vijana uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto.
Aisa maendeleo ya jamii anayeshughulika na vijana ndugu Rodrick Kidenya akiwasilisha ombi la vijana kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto kuwa mlezi wa SACCOS ya vijana.
Vijana wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mh. Lairumbe Mollel,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamim Kambona,Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii ndugu Joseph Mwaleba,mkuu wa idara ya Kilimo ushirika na umwagiliaji ndugu Robert Urassa,afisa ushirika ndugu Joseph Mwanga, afisa maendeleo ya jamii anayeshughulika na vijana ndugu Rodrick Kidenya na uongozi wa muda wa Kiteto Vijana SACCOS baada ya uzinduzi wa SACCOS hiyo uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto.
Vijana wakisikiliza kwa makini maelekezo baada ya uzinduzi wa SACCOS yao uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto
HABARI KAMILI
Halmashauri ya wilaya ya Kiteto yazindua SACCOs ya vijana .
Halmashauri ya wilaya ya kiteto imezindua SACCOs ya vijana wa wilaya ya kiteto . Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ambapo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto mheshimiwa Lairumbe Mollel amemkabidhi mwenyekiti wa muda wa bodi ya SACCOS hiyo ndugu Hamza Ally cheti cha usajili ,sera na katiba ya SACCOs hiyo ambayo itajulikana kwa jina la Kiteto Vijana SACCOs .
Aidha mheshimiwa Mollel amewapongeza vijana kwa kujiunga na SACCOs , amesema kuna maagizo ya waziri mkuu kwamba katika kuchagua viongozi wa vyama vya ushirika mtu yeyote ambaye alikuwa kwenye ushirika huko nyuma asichaguliwe kuwa kiongozi, kwa sababu imeonekana kwamba walifanya vibaya, wawachague viongozi wazuri , ambao watasimamia vizuri fedha watakazokuwa wanapewa na halmashauri.Pia amewaasa kufuata sheria na taratibu za SACCOs katika kukopeshana na sio kukopeshana kwa urafiki au undugu na kutoingiza siasa katika undeshaji wa SACCOs yao kwani vyama vya ushirika havitaki siasa.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamim Kambona amempomngeza afisa ushirika kwa bidii aliionyesha katika kuhakikisha usajili wa SACCOs ya vijana inakamilika kwa wakati.Pia amewapongeza vijana kwa maamuzi mazuri ambayo wamefanya.Mkurugenzi amesema’’ Sisi kama halmashauri tunapata changamoto sana kwenye ukopeshaji wa fedha za vijana na wanawake,ndio maana mimi mwaka jana niliamua kubadili utaratibu, badala ya kutoa fedha tukawakopesha pikipiki vijana, lakini tumewakopesha hizo napo tumekutana na changamoto nyingine nyingi zaidi mpaka sasa hivi tumefikia hatua ya kunyang’anya zile pikipiki wengine.Sasa uanzishaji wa SACCOs kwa sababu imesajiliwa rasmi na ina taratibu zake, ina katiba na kila kitu.Nafikiri sasa tumepata sehemu ambayo ni salama zaidi.Na mimi nimewaambia hata wakuu wa idara kwamba kuanzia sasa sitatoa fedha za mikopo ile ya vijana tena kwenye vikundi,hiyo imekufa.Fedha zote za vijana ile asilimia tano tutapeleka kwenye SACCOs tu ya vijana.Kwa sababu ni SACCOs ya vijana na iko wilaya nzima,kwa hiyo tushauri vijana wote wale waliokuwa wagumu kujiunga katika vikundi,waje kujiunga na SACCOs.Wasipojiunga, ule utaratibu wa kuwapa pikipiki haupo tena.Kwa hiyo tunategemea kwamba kuanzia mwezi ujao tuanze kuwaingizia fedha na ninyi muanze kukopesha vijana wenzenu.Pia mkurugenzi amewataka vijana kutobweteka bali waongeze jitihada ili SACCOs yao iweze kuwa na mvuto zaidi.
Naye Afisa kilimo umwagiliaji na ushirika wa wilaya ya Kiteto ndugu Robert Urassa amewapongeza vijana kwa kuona umuhimu wa kujiunga na SACCOs, na kutoa angalizo kwamba SACCOs hiyo ni ya vijana na sio kikundi cha vijana,na kwamba SACCOs zina utaratibu wake, hivyo ni matumaini yake kwamba watu wa maendeleo ya jamii hawataingilia utaratibu wa uendeshaji wa SACCOs hiyo kwani SACCOs ziko chini ya maafisa ushirika.Pia ndugu Urassa amesisitiza kwamba mpango wa halmashauri ni fedha zote za vijana kupelekwa kwenye SACCOs na zitatolewa kulingana na taratibu na sheria za SACCOs, na ana matumaini makubwa na SACCOs hiyo kwamba italeta manufaa makubwa kwa vijana na kuwawezesha kutekeleza azma ya hapa kazi tu .
Akitoa maelekezo kuhusu utaratibu wa uendeshaji wa SACCOs, Afisa ushirika ndugu Joseph Mwanga amesema kwamba SACCOs hiyo imeanzishwa kisheria hivyo jambo lolote watakalo lifanya lazima wafuate sheria, watakapoamua kufanya kitu chochote kile,iwe ni kupokea fedha au kutoa fedha kwa mwanachama ,namna ya kukopesha imeandikwa katika sera ya mikopo na kwamba sheria zinazowasimamia ziko ndani ya sheria ya vyama vya ushirika ambayo imepititishwa na matawi ya vyama vya ushirika ,na ndiyo katiba yao,na kwamba inasimama hata mahakamani kutoa maamuzi kwenye mambo ambayo watayafanya. Ndugu mwanga amesisitiza kwamba ni lazima wazingatie kile ambacho wamepewa, lakini pia katika kuandikishwa kuna masharti na miongozo ambayo wamepewa, wamepewa kwa maandishi, waipitie wakishaipitia ndiyo itakayowaongoza nini wafanye na kwamba uongozi uliopo ni wa mpito, sheria inasema kwamba uongozi uliopo sasa ni uongozi wa mpito , wameandikiwa kwamba lazima waingie kwenye mchakato wa kuchagua uongozi rasmi, ambao utakuwa ni uongozi baada ya kuandikishwa. Na ndiyo utakaofanya shughuli zote za kisheria zinazotambulika ambazo zipo ndani ya utaratibu wa sheria mama ya ushirika.Baada ya kujaza fomu uongozi huo utavunjwa rasmi na utachaguliwa uongozi ambao upo ndani ya utaratibu wa vyama vya ushirika.
Katika hatua nyingine afisa maendeleo ya jamii anayeshughulika na vijana ndugu Rodrick Kidenya aliwasilisha ombi la vijana kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Kiteto la kuwa mlezi wa SACCOs ,ombi ambalo Mkurugenzi alisema ‘’nimelipokea kwa mikono miwili,na kwa sababu kazi hii mmenikabidhi mimi, sitaki lelemama, sitaki usanii usanii ,tusimame kweli ili ifahamike kitaifa kwamba kweli Kiteto kuna SACCOs ya vijana , nitahakikisha fedha zenu zinakuja kwa wakati’’.
SACCOs hiyo itaendeshwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa , kwa sasa SACCOs ina uongozi wa muda ambao uliteuliwa ili kuhakikisha kwamba inasimama, hivyo baada ya uzinduzi na ujazaji wa fomu, uongozi kamili utateuliwa ambapo kutakuwa na bodi, kamati ya SACCOs,meneja na mhudumu .
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa