Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kiteto ndugu Emmanuel Mwagala akiogoza zoezi la upimaji VVU kwa watumishi wa umma wilayani Kiteto
Watumishi wa umma wilayani Kiteto wakiwa katika zoezi la upimaji VVU
Watumishi wa umma wilayani Kiteto wakiwa katika chumba cha kupokelea majibu baada ya kupima VVU
Wataalamu wa afya kutoka katika hospitali ya wilaya ya Kiteto wakiendesha zoezi la upimaji VVU kwa watumishi wa umma wilayani Kiteto
Habari kamili......
Halmashauri ya wilaya ya Kiteto yaendesha zoezi la upimaji VVU kwa watumishi wa umma wilayani Kiteto
Halmashauri ya wilaya ya Kiteto imeendesha zoezi la upimaji wa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa watumishi wa umma wilayani Kiteto. Zoezi hilo limefanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto na limeendeshwa na wataalamu wa afya kutoka hospitali ya wilaya ya Kiteto.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Emmanuel Mwagala amesema kwamba zoezi hilo la upimaji wa VVU kwa watumishi ni agizo la wizara ya afya, kwamba watumishi wahamasishwe kupima ili kujua hali ya maambukizi kwa watumishi. Aidha amesema kwamba ni muhimu watumishi kupima ili kujua hali ya afya zao, kwani wakishapima na kujua hali zao wanaweza kuchukua tahadhali mapema . Kaimu mkurugenzi huyo ameongoza zoezi hilo la upimaji VVU na kutoa rai kwa watumishi wote kwamba ni vema watumishi wapime , ili wajue hali ya afya zao , hiyo itawasaidia kujua namna ya kuishi na kuweka mipango yao ya maisha baada ya kujua hali zao za afya, kwani kinga ni bora kuliko tiba.
Akizungumza kwa niaba ya wataalamu wa afya wanaoendesha zoezi hilo la upimaji VVU ndugu Pili Casian amesema kwamba muitikio ni mzuri ,idadi ya watumishi wanaofika kupima ni ya kuridhisha .
Katika hatua nyingine watumishi waliohojiwa kuhusu zoezi hilo wamesema kwamba zoezi hilo ni muhimu sana katika kujua hali yamaambukizi , ili serikali kupitia wizara ya afya iweze kuweka mikakati ya jinsi ya kupambana kupunguza kasi ya maambukizi mapya. Vilevile ni muhimu kwani mtu anapokuwa amepima ,kama hana maambukizi inamfanya kuwa makini na mienendo yake, akiwa hajapima anaishi bila ya kuwa na uhakika wa hali ya afya yake, jambo ambalo ni hatari kwani yawezekana akawa hajaambukizwa lakini kutokana na kutokujua hali ya afya yake asichukue tahadhari na hivyo kumsababishia kupata maambukizi. Pia kama mtu atakuwa amekutwa na maambukizi ataweza kuwahi kutumia dawa kabla afya yake haijadhoofu na itamsaidia kujua kwamba ataishi namna gani ili afya yake iendelee kuwa imara.
Zoezi hilo la upimaji VVU kwa watumishi linaendelea hadi tarehe 11/11/2017 ambapo idadi ya watumishi waliokutwa na maambukizi pamoja na majina ya watumishi wote waliopimwa yatapelekwa mkoani kwa ajili ya kuyaunganisha na majina mengine ya watumishi kutoka wilaya zote za mkoa wa manyara na kupelekwa wizara ya afya .
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa