Zoezi hili lilianza tarehe 10.04.2017 hadi 25.04.2017 ambapo baadhi ya wataalamu wa Idara ya Elimu ya Msingi, Elimu ya Sekondari, Utumishi na Utawala na Kitengo cha Tehama walihusika kuhakikisha takwimu hizo zinapandishwa na kukamilika kwa wakati katika Mfumo huo.
Kimsingi takwimu hizi kwa Elimu ya Shule za Msingi ni 90 ( kati ya hizo 87 ni za Serikali na 3 ni za Binafsi ) Elimu ya Awali 88 (kati ya hizo 85 ni za Serikali na 3 ni za Binafsi) na mwisho ni Elimu ya Watu wazima ambapo ni jumla ya vituo 20 kwa Wilaya nzima.
Wakati, Elimu ya Sekondari ni Shule 17 ( kati ya hizo 16 ni za Serikali na 1 ni ya Binafsi )
Dhumuni kuu la kupandisha takwimu hizi katika Mfumo huu ni kuiwezesha Serikali kujua changamoto za kielimu kwa kila Shule na Wilaya ili zisaidie katika maamuzi sahihi "Sound Decisions" ya kimaendeleo kwa kupanga mikakati endelevu itakayowezesha upangaji na uwezeshaji wa rasilimali za nchi kulingana na ukubwa wa changamoto ya Wilaya husika kupitia bajeti kuu ya Serikali kwa shabaha kuu ya kumletea maendelea mwananchi na Taifa kwa ujumla wake.
Takwimu hizi zote zimepandishwa na kumalizika kwa wakati kwa uwezeshwaji wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) katika upatikanaji wa Vifaa vya kufanyia kazi na ufuatiliaji wa karibu.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa