Uzio wa hospitali ya wilaya ya Kiteto unaojengwa na halmashauri ya wilaya ya Kiteto unavyoonekana pande zote
Halmashauri ya wilaya ya Kiteto yajenga uzio wa hospitali ya wilaya
Halmashauri ya wilaya ya kiteto inajenga uzio wa hospitali ya wilaya.Uzio huo ambao kwa kiasi kikubwa uko katika hatua za mwisho,unajengwa kwa kutumia mapato ya ndani ya halmashauri .
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Kiteto daktari Ramadhani Maingu amesema kwamba uzio huo utakapokamilika utaimarisha ulinzi katika eneo la hospitali kwani kwa hali ilivyo sasa watu wamekuwa wakiingia na kutoka eneo la hospitali kwa kupitia maeneo yaliyo wazi , hivyo kuhatarisha usalama wa mali za hospitali na kuleta usumbufu kwa watumishi wa hospitali hiyo wakati wakitekeleza majukumu yao. Pia baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakitoroka hospitali kwa kupitia maeneo hayo .
Aidha Katibu wa afya wa wilaya ya Kiteto ndugu Dia Ally amesema kwamba uzio huo wa hospitali ni muhimu sana katika kudhibiti maambukizi kwani bila ya kuwa na uzio wanyama kama mbwa wanakuchukua taka hatarishi na kuzipeleka kwenye makazi ya watu jambo ambalo linaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa.Kadhalika watoto wanaokota taka hizo,hali ambayo ni hatari kwani inaweza kuwasababishia maambukizi ya magonjwa. Vilevile Katibu wa afya wa wilaya amesema kwamba uzio huo utasaidia katika kudhibiti watu kuingia maeneo ya hospitali nje ya muda maalumu uliowekwa, kwani watu wanaokuja kuangalia wagonjwa wanatakiwa kuingia hospitali kwa muda maalum ili kutoa nafasi kwa watumishi kuweza kutekeleza majukumu yao kwa utulivu.
Nao Wauguzi wa hospitali ya wilaya ya Kiteto walipohojiwa kwa nyakati tofauti wamesema kwamba wamefurahishwa sana na ujenzi wa uzio huo, kwani utakapokamilika utasaidia kuondoa usumbufu wa ndugu na jamaa ambao wamekuwa wakiingia wodini kuwaona wagonjwa katika muda usioruhusiwa kwa kupitia maeneo yasiyokuwa na uzio.Pia kukamilika kwa uzio huo kutaongeza usalama wa vifaa vya hospitali hiyo.
Katika hatua nyingine walinzi wa hospitali hiyo wamesema kwamba wanashukuru sana kwa ujenzi wa uzio huo kwani utakapokamilika utasaidia kuondoa adha wanayoipata sasa ya watu kuingia katika maeneo ya hospitali bila utaratibu hususani nyakati za usiku, jambo ambalo linahatarisha usalama wa wagonjwa na mali za hospitali na linaleta usumbufu mkubwa sana kwa wagonjwa na kwao pia.
Ujenzi huo ambao unaendelea kwa kasi kubwa, mpaka sasa umegharimu kiasi cha shilingi milioni ishirini na laki tano(2,500,000).Hata hivyo ujenzi wa Uzio huo pamoja na miradi mingine inayoendelea kutekelezwa wilayani Kiteto inatokana na jitihada za Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamimu Kambona ambaye amedhamiria kuleta maendeleo ya kweli wilayani kiteto akishirikiana na wakuu wa idara za halmashauri ya wilaya ya Kiteto .
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa