• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Yapania Kuongeza Ufaulu Wilayani Kiteto.

Imetumwa : July 27th, 2017

Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Kiteto Bw. Tamim H. Kambona  akimkabidhi fedha Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto  Mhe. Lairumbe  Mollel kwa ajili ya kuzizawadia  shule  zilizofanya  vizuri katika  Mitihani  ya Taifa ya darasa la saba  na  kidato  cha  nne  mwaka 2016.




Walimu wa shule zilizofanya vizuri katika mitihani ya taifa ya  darasa la saba na kidato cha nne mwaka 2016 wakikabidhiwa fedha na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mhe. Lairumbe Mollel. Fedha hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa wilaya ya Kiteto Bw. Tamim H. Kambona kama zawadi kwa shule hizo.

HABARI KAMILI...

Halmashauri  ya  wilaya ya Kiteto imepania kuongeza ufaulu  katika mitihani ya taifa kwa shule za msingi na sekondari mwaka  2017  wilayani Kiteto . Afisa elimu shule za msingi wilaya ya Kiteto  bwana  Emmanuel Mwagala amesema kwamba lengo la mkoa wa  Manyara ni  kufaulisha wanafunzi kwa asilimia themanini,na kwamba halmashauri ya wilaya ya kiteto chini ya  Mkurugenzi wake makini  bwana Tamim Kambona wamejipanga vema katika  kuhakikisha kwamba lengo hilo linatimia kwa kuweka mikakati madhubuti ambapo  idara ya elimu shule za msingi  kwa kutumia maafisa elimu,waratibu elimu kata na walimu  wakuu wa shule  wanawajibika kufuatilia kwa karibu sana ufundishaji katika shule zote, kuhakikisha kwamba walimu wanawapa wanafunzi mazoezi  ya mara kwa mara na mitihani mingi ya kujipima ili kuwaongezea uzoefu wa kujibu maswali ya mitihani ya taifa na  kuwafanya  wasome kwa bidii,  pia  walimu wakuu wa shule  na waratibu elimu kata  wameweka mkataba na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto wa kufikisha ufaulu wa asilimia themanini kwa kula  kiapo cha kutimiza lengo hilo.


Aidha bwana Mwagala amesema kwamba tarehe  30/05/2017 hadi tarehe 01/06 /2017    wanafunzi wa darasa la saba  mkoa wa Manyara walifanya mitihani ya utamilifu (Mock )ambapo kwa wilaya ya Kiteto matokeo  yamekuwa mazuri sana  yakilinganishwa na matokeo  ya mwaka jana (2016), ambapo ufaulu ulishuka kidogo. Katika mitihani hiyo ya utamilifu  2017 wilaya ya Kiteto imeshika nafasi ya kwanza kwa ufaulu wa jumla, katika shule kumi bora wilaya  imetoa shule tano. Kwa upande wa wanafunzi kumi (10)  bora wasichana, wilaya  imetoa wanafunzi tisa (9) na kwa wanafunzi kumi (10)  bora   wavulana wilaya  imetoa wanafunzi watano(5) . Nafasi hiyo ya ufaulu  imekuwa  faraja sana na kuongeza ari  kwa Mkurugenzi wa halmashauri pamoja na idara ya elimu katika kuweka mikakati zaidi ili kufikisha na kuvuka  lengo la  ufaulu wa asilimia themanini. Shule zilizofanya vizuri  katika mitihani hiyo  ni Laalakir, Umoja, Boma, Sunya, Olchanyodo, Bwawani, Shekina,Nati, Lobosoiti na Azimio.  Bwana Mwagala amesema kwamba shule ya msingi Laalakir imeendelea kufanya vizuri  kwa miaka minne (4) mfululizo na kwamba wameweza kutunza nafasi yao ya ufaulu kwa kushika nafasi ya kwanza kwa miaka yote hiyo.


 Kwa upande wa idara ya elimu Sekondari  kaimu afisa elimu shule za sekondari  wilaya ya Kiteto bwana Mtinga Maleya amesema kwamba  wamejipanga kuongeza ufaulu kufikia lengo la  mkoa la ufaulu wa asilimia themanini kwa   kuweka mikakati ambayo ni kuhakikisha kwamba idara ya elimu sekondari wanafuatilia kwa karibu ufundishaji mashuleni. Kuhakikisha kwamba kuna mahudhurio mazuri darasani kwa walimu na wanafunzi, kuhakikisha kwamba walimu wanatoa mazoezi kila wiki na kila mwezi na mitihani ya utamilifu (Mock) inafanyika pamoja na  kuhakikisha kwamba  kunakuwa na upatikanaji samani(viti na meza)  za kutosha ili wanafunzi waweze kukaa vizuri darasani wakati wanafundishwa. Aidha bwana Maleya amesema kwamba mikakati hiyo inatekelezwa kwa  maafisa elimu kukaa na walimu kuangalia kazi wanazozifanya, ikiwemo ufundishaji, mazoezi na majaribio ya kila wiki na kila mwezi wanayotoa,  kuangalia mafanikio na changamoto zinazowakabili katika ufundishaji  na kuzifikisha katika mamlaka husika kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi, kufuatilia mahudhurio ya walimu na wanafunzi madarasani pamoja na kuangalia mgawanyo wa vipindi kwa walimu. 


Aidha Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto ametoa mafuta kuhakikisha kwamba  idara ya elimu  wanafanya kazi ya kutembelea shule zote mara kwa mara kufuatilia na  kuhimiza ufundishaji,utoaji wa mazoezi na mitihani mingi yakujipima ili kuiwezesha wilaya kupata matokeo mazuri zaidi katika mitihani ya taifa ya mwaka  2017. Pia mkurugenzi  ametoa zawadi kwa shule za msingi na sekondari  zilizofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2016 kama  motisha ya kufanya bidii ili kuendelea kupata  ufaulu mzuri zaidi ambapo shule ya  msingi Laalakir  imezawadiwa  shilingi  milioni  moja, shule  ya  msingi  Boma  imezawadiwa  shilingi  laki  tano  na Shule  ya  msingi  Shekina  imezawadiwa    shilingi  laki  saba. Shule ya sekondari Kibaya  imezawadiwa  shilling milioni moja na shule ya sekondari Eko   imezawadiwa    shilingi  laki saba. Kiasi  hicho  cha fedha kimetolewa  kwa   shule  kulingana na  vigezo  vilivyotumika  kikiwemo kigezo cha  idadi  ya wanafunzi  katika shule hizo, na idadi ya wanafunzi ambayo  shule hizo zimefaulisha.


Hata hivyo pamoja na jitihada zote hizo za kuongeza ufaulu idara ya elimu inakabiliwa na changamoto  za  upungufu  wa  vyumba   vya  madarasa 400,  nyumba  za walimu, ambapo walimu wanaishi mbali sana na shule wanakofundisha,na upungufu wa walimu 200.




Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPTEMBA 2023 September 03, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABIA MBAYA ZA WATUMUSHI ZINAHARIBU SIFA ZA TAASISI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LIMEMPONGEZA RAIS SAMIA.

    May 30, 2025
  • PONGEZI KWA WANANCHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

    April 28, 2025
  • TUUENZI MUUNGANO WETU

    April 27, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa