Makamu mwenyekiti aliyemaliza muda wake Mh. Yahya Masumbuko akibadilishana joho na makamu mwenyekiti mteule Mh. Hassan Benzi mara baada ya uchaguzi uliofanyika katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto
Makamu mwenyekiti aliyemaliza muda wake Mh. Yahya Masumbuko akiwashukuru wajumbe wa baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto na kumkaribisha makamu mwenyekiti mpya mara baada ya uchaguzi uliowezesha kupatikana kwa makamu mwenyekiti mpya wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto
Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mh. Tumaini Magessa akitoa maelekezo ya Serikali katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto.Mkuu wa wilaya alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho .
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mh. Lairumbe Mollel akizungumza na wajumbe wa baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Ndg. Tamim Kambona akifafanua jambo katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto
Mbunge wa jimbo la Kiteto Mh.Emmanuel Papian akichangia hoja katika kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
Wajumbe wa baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto wakipiga kura kuchagua makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto
Wajumbe wa baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto wakifuatilia kwa makini taarifa za kamati za halmashauri.
Mweka hazina wa wilaya ya Kiteto Ndg. Nassoro Mkwanda akiwasilisha taarifa ya mapato na matumizi katika kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kiteto.
Afisa utumishi wa wilaya ya Kiteto Ndg. Rafael Makoninde akiwasilisha hoja za watumishi katika baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
HABARI KAMILI
Halmashauri ya wilaya ya Kiteto yapata makamu mwenyekiti mpya
Halmashauri ya wilaya ya Kiteto imepata makamu mwenyekiti mpya baada ya uchaguzi uliofanyika katika Kikao cha baraza la madiwani cha tarehe 29 na 30 Agosti 2017.Katika kikao hicho ajenda kuu ilikuwa ni uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ambapo vyama vya CUF na CHADEMA vinavyounda ukawa havikuweka mgombea, hivyo mgombea wa CCM mheshimiwa Hassan Benzi akachaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa halmashari kwa kura 30 kati ya kura 31 zilizopigwa.
Aidha mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya kiteto mheshimiwa Lairumbe Mollel aliwatangaza diwani wa Sunya mheshimiwa Musa Brighton kuwa mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii,diwani wa Partimbo Paul Tunyoni kuwa mwenyekiti wa kamati ya uchumi ,ujenzi na mazingira na diwani wa lengatei Mainge Lemalali kuwa mwenyekiti wa kamati ya maadili.
Katika wajumbe wanne wanaoteuliwa na mwenyekiti,mheshimiwa Mollel aliwateua mheshimiwa Nganisi Meshack,mheshimiwa Rehema Chileleo,mheshimiwa Yahaya Masumbuko na mheshimiwa Kidawa Iyavu.Mheshimiwa Mollel aliwataka madiwani kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo inayofanyika kwenye kata zao,ili iendane na thamani ya fedha zinazotumika.Pia aliwataka watendaji wa serikali kukusanya mapato.
Katika hatua nyingine mgeni rasmi katika kikao hicho mkuu wa wilaya ya Kiteto Mheshimiwa Tumaini Magesa aliwataka waheshimiwa madiwani na watumishi wote wa umma kujiandaa vema kuupokea mwenge wa uhuru ambao utapokelewa wilayani Kiteto tarehe 13/09/2017. Mkuu wa wilaya pia alielekeza juu ya matumizi bora ya ardhi ,kwamba kila kijiji kiweke mpango wa matumizi bora ya ardhi,na kwamba kinapoweka mpango huo kishirikishe vijiji vya jirani ili kuondoa kutofautiana katika matumizi na kuleta migogoro baina ya vijiji.Pia alitoa maelekezo juu ya kuwepo na madaftari ya wakazi , kila kijiji kiwe kinaandikisha wakazi wake katika daftari ili kuwatambua wakazi wa eneo husika na kuwabaini wageni wanaoingia vijijini na kuvamia maeneo.
Mkuu wa wilaya ametoa angalizo kuhusu sumukuvu,kwamba inatishia maisha ya watu kwani watoto watano wameathirika na sumu kuvu ambapo watatu kati yao walifariki, kuwaelekeza madiwani kuwasisitiza wananchi wao kufuata taratibu walizoelekezwa na wataalamu katika kuhifadhi mazao yao ya chakula.Mkuu wa wilaya pia amezungumzia kuhusu ukosefu wa shule katika vijiji viwili ndani ya halmashauri ya wilaya ya kiteto ambavyo ni kijiji cha Lareg na Ngapapa,ambapo ameelekeza kwamba baada ya ujio wa mwenge madiwani wote pamoja na yeye mkuu wa wilaya kufanya ziara katika vijiji hivyo ili kujionea hali halisi na kuweka mikakati ya kujenga shule katika maeneo hayo.Kuhusu suala la mimba mashuleni, mkuu wa wilaya amesema kwamba bado ni changamoto kwani katika mwaka 2016 /2017 jumla ya wanafunzi 156 waliacha shule kutokana na kupata mimba hivyo amewataka madiwani kushirikiana naye katika mapambano ya kuondoa tatizo hilo kwa kukemea vitendo vinavyosababisha mimba mashuleni kuendelea katika kata zao.
Aidha shughuli za kawaida za baraza ziliendelea kulingana na ajenda zilizokuwepo ambapo taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka kwenye kata kwa robo ya nne April – June 2017) zilipokelewa, zilisomwa na kuthibitishwa .Muhtasari wa mkutano wa kawaida wa halmashauri uliopita ulisomwa na kuthibitishwa . Maswali yalijibiwa kufuatana na kanuni ya 21 ya kanuni za mikutano ya halmashauri. Taarifa za kamati ; kamati ya fedha, uongozi na mipango,kamati ya huduma za jamii (elimu, afya na maji) na kamati ya huduma za uchumi(ujenzi,mazingira,kilimo na mifugo) zilipokelewa kutoka kwa wenyeviti wa kamati na kujadiliwa.Kila kamati ilitoa taarifa yake na ilipokelewa ,ilijadiliwa na kupitishwa.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa