Septemba 25, 2025, Halmashauri ya Wilala ya Kiteto imeendesha semina elekezi kwa kamati za ujenzi na kamati za mapokezi zinazohusika moja kwa moja katika usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali.
Lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati hizo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, uwazi na uwajibikaji, sambamba na kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa inalingana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali.
Wakati wa mafunzo hayo, wajumbe wamekumbushwa kuzingatia kikamilifu kanuni, sheria na taratibu za usimamizi wa miradi ya umma, kuepuka matumizi mabaya ya fedha, pamoja na kuhakikisha ubora na viwango vinazingatiwa katika kila hatua ya utekelezaji wa miradi.
Aidha, wajumbe wamefundishwa majukumu yao ya msingi ikiwemo kusimamia utekelezaji wa miradi, kutoa taarifa za maendeleo ya mradi.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa