Wahenga walisema "Hayawi hayawi sasa yamekua". Kile kilio cha muda mrefu cha wananchi wa kata ya Kaloleni cha kupata shule mpya ya msingi sasa kimesikiwa na hatimaye kata hiyo inaenda kupata shule yenye thamani ya shilingi milioni 330.7 kutoka serikali kuu kupitia programu ya BOOST.
Akizungumza siku ya Julai 29,2025 mbele ya wananchi wa kata hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Erasmo Tellun Ndelwa amesema kwamba katika mwaka wa fedha 2025/26 halmashauri imepokea kiasi hicho cha fedha kwaajili ya mradi wa ujenzi wa miundombinu muhimu ya shule ikiwa ni pamoja na: madarasa sita (06) ya elimu ya msingi, madarasa mawili (02) ya mfano kwa elimu ya awali, matundu ya vyoo sita (06) kwa wanafunzi wa elimu ya msingi na matundu sita(06) ya vyoo kwa wanafunzi wa awali.
Aidha, ujenzi huo utahusisha vyoo matundu mawili (02) kwaajili ya walimu pamoja na jengo moja la utawala.
Nae Afisa kutoka TAKUKURU Ndg. EliBrighton Mmari amesema kwamba taasisi hiyo itakua macho katika utekezaji wa mradi huo na amewaasa wananchi kuwa walinzi wa mradi huo.
"Kuna wananchi wamechaguliwa kwenye kamati za utekelezaji wa mradi huu lengo ni kuhakikisha wananchi wanashiriki vizuri katika mradi pia kuongeza uwazi" Aliongeza Ndg. Mmari.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Mwema Emmanuel amewaasa wajumbe wa kamati ya ujenzi wa mradi huo kuhakikisha wanawatafuta wazabuni ambao wana uwezo wa kuleta vifaa kwa wakati kwasababu ucheleweshwaji wa vifaa kutafanya mradi kutokamilika kwa wakati.
Sambamba na hayo alisisitiza juu ya mafundi na kutia mkazo kua wahakikishe wafundi wanaopewa tenda ni wale wenye uwezo.
"Sita sita kumchumkulia hatua yoyote atakaye leta mchezo kwenye mradi huu nawakumbusha Mafundi kuwa makini katika Utekelezaji wa Mradi huu alisisitiza Mhe. Mwema.
Mhe. Mwema aliwaeleza wananchi wa kata hiyo kua wamekua wakiomba shule kwa muda mrefu na hatimaye serikali sikivu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais. Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imewapelekea fedha kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo mpya.
"Tuna kila sababu ya kumshukuru Dr. Samia kwa fedha hizi.", aliongeza Mhe. Mwema.
Nao wananchi wa kata hiyo walimuomba Mhe. Mwema kufikisha salamu zao za shukrani kwa Mheshimiwa Dkt. Samia kwa kuwatatulia kero hiyo ambayo imedumu kwa mda mrefu.
Kukamilika kwa ujenzi wa shule hii kutasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya Msingi Kaloleni.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa