Wananchi wa Kiteto na Watanzania kwa ujumla wameaswa kuzingatia haki za watoto na kuwa mstari wa mbele kupambana na kupinga ukatili dhidi ya watoto.
Rai hiyo imetolewa Juni 16,2025 na Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Ndg. Mufandii Msaghaa, katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Compassion kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Ndg. Msaghaa ambaye alikua Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo, aliwakumbusha wazazi na walezi juu ya wajibu wao wa malezi bora na kuwajenga watoto katika maadili na kuwataka kuwa makini na matumizi ya teknolojia kwa watoto haswa simu na kompyuta kwani zinachangia kuharibu maadili ya watoto endapo watoto wanazitumia pasipo uangalizi makini wa wazazi au walezi.
Nae Mchungaji Sarah Weki Mbelwa, amewasisitiza watoto kuwa watii kwa walimu na wakubwa pamoja na kuwa watii kwa sheria za shule na sheria za nchi.
Katika maadhimisho hayo, Afisa kutoka Dawati la Jinsia Polisi, aliikumbusha jamii kuhusu sheria ya mtoto,matunzo pamoja na wajibu wa kuwasomesha watoto.
Kauli mbiu: Haki za mtoto, Tulipotoka, Tuliko na Tuendako.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa