Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 Kitaifa, Ndg. Ismail Ali Ussi, amelipongeza Jeshi la Polisi Wilayani Kiteto kwa jitihada wanazofanya katika kupambana dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya wilayani hapa na kuwasihi polisi waendeelee kufanya jukumu lao la kudhibiti dawa za kulevya.
Pongezi hizo zimetolewa Julai 13, 2025, mara baada kusomewa taarifa dhidi ya mapambano ya matumizi ya dawa za kulevya wilayani hapa, taarifa ambayo ilisomwa katika Viwanja vya Sekondari ya Ndedo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kuwasili wilayani hapa.
Taarifa hiyo imesema kwamba Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekua wakitoa elimu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya hususani kwa kundi la vijana ambao ndio wahanga wakubwa.
Aidha Jeshi la Polisi limeendelea kufanya doria na misako ili kudhibiti uingizaji wa dawa za kulevya kutoka katika mikoa na wilaya za jirani. Katika kipindi cha kutoka Juni 2024 hadi Juni 2025 Jeshi la polisi wilayani hapa limefanikiwa kukamata bangi yenye uzito wa kg 3.26, misokoto 07, kete 12 na miche 12 pamoja na mirungi yenye uzito wa kg 130.
Kutokana na madawa hayo yaliyokamatwa, jumla ya kesi 14 zilifunguliwa katika vituo vya polisi na watuhumiwa 8 walikamatwa na kesi 08 zilifikishwa mahakamani ambapo kesi 04 kati ya hizo zilipata mafanikio kwa watuhumiwa kuhukumiwa vifungo gerezani, kesi 03 zinaendelea mahakamani, kesi 01 ilishindwa mahakamani na kesi 06 zipo chini ya upelelezi kwa watuhumiwa kutopatikana
Dawa hizo zilizokamatwa zililetwa katika viwanja hivyo na kuteketezwa kwa moto na Kiongozi wa Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru 2025.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa