Mkuu wa Wilaya wa Kiteto, Mhe. Remidius Mwema, ametoa rai kwa wananchi wa Kiteto kujitokeza kwenye vituo vya uandikishaji kwaajili ya kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili waweze kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025.
Rai hiyo imetolewa leo Septemba 25, 2024 katika Ofisi za Kata ya Kibaya alipoenda kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mapema leo, mara baada ya kituo hicho kufunguliwa, Mkuu huyo wa wilaya aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kiteto CPA. Hawa Abdul Hassan pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. Mufandii Msaghaa ambapo viongozi wote hao walikua miongoni wa wananchi walioboresha taarifa zao kwenye kituo hicho.
"Ninawapongeza kwa kujitokeza kuja kuboresha taarifa zenu. Niwaombe muwe mabalozi kwa wengine ili nao waweze kuja kuboresha taarifa zao. Ila pia kuna vijana wetu ambao sasa hivi wana miaka 17 hao wanapaswa kujiandikisha kuwa wapiga kura kwani ifikapo tarehe ya Uchaguzi Mkuu 2025 watakua wameshatimiza miaka 18", ameongeza Mhe. Mwema.
Nae Mkurugenzi Mtendaji (W), CPA. Hawa, ametoa wito kwa wananchi ambao ndugu zao wamefariki na waliwahi kujiandikisha kuwa wapiga kura, waende kwenye vituo vya uandikishaji na taarifa za marehemu ili taarifa zao ziondolewe kwenya Daftari.
Zoezi la Uboreshwaji Jimboni Kiteto, ambalo limeanza Septemba 25, 2024 linatarajiwa kukamilika Oktoba 1,2024.
Vituo vyote vya uandikishaji vinafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
"Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora".
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa