Kamati ya Fedha, Uratibu na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto imefanya ziara ya siku mbili kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Makame.
Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo Aprili 23, 2025, katika kata ya Lengatei, Kamati imetembelea mradi wa ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na choo matundu 12 katika shule ya Msingi Kurash pamoja na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya choo katika shule ya Msingi Malimogo.
Aidha katika siku hiyo Kamati ilitembelea ujenzi wa choo cha wasichana matundu matano na chumba maalumu kimoja katika shule ya Sekondari Loolera, ukamilishaji wa ujenzi wa Soko la Sunya na ukamilishaji wa jengo la mama na mtoto, jengo la kufulia, jengo la upasuaji na ujenzi wa korido kuunganisha majengo hayo na jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Kituo cha Afya Kijungu.
Katika siku ya pili ya ziara hiyo April 24, 2025 kamati ilifika katika kata ya Makame na kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Msingi Ilkiushbor pamoja na ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Makame.
Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Mhe. Abdallah Bundala, amehimiza miradi ambayo haijakamilika kukamilika mapema ili kuiwezesha jamii kunufaika na miradi hiyo ambayo serikali imetoa fedha nyingi.
Aidha Mhe. Bundala amesisitiza matumizi sahihi ya fedha za umma na kusisitiza usimamizi makini wa miradi hiyo na kuahidi kuwa kamati itaendelea kuifuatilia miradi hiyo hadi ikamilike.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa