• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Kamati ya Lishe Yataka Ufuatiliaji wa Karibu Katika Bidhaa na Huduma za Vyakula

Imetumwa : January 15th, 2019

Wajumbe wa kamati ya lishe wakiendeklea na kikao

Mwenyekiti( Christopher Simwimba aliyeko kushoto) na katibu wa kikao ( Dkt. Paschal Malkiad Mbota aliyekaa kulia)  wakifuatilia kwa makini majadiliano kuhusu taarifa zilizowasilishwa kwenye kikao cha kamati ya lishe.

Wajumbe wa kamati wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuuli za lishe.



.........HABARI KAMILI..............




Kamati ya lishe wilaya ya Kiteto imeitaka idara ya afya na usafi wa mazingira kufuatilia  kwa karibu biashara zote zinazohusisha bidhaa za vyakula, ili  kuipeusha jamii na madhara yatokanayo na ulaji wa vyakula vilivyoisha muda wake, na vilivyotayarishwa na kuhifadhiwa katika hali isiyo salama.Azimio hilo limeafikiwa katika kikao cha kamati ya lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto asubuhi ya leo  tarehe 15.01.2019.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti  wajumbe wa kamati ya lishe wamesema kwamba ziko bidhaa ambazo hata muda wake wa matumizi hauonekani,vilevile wamezungumzia kuhusu uhifadhi wa vyakula na huduma ya chakula kwa ujumla  katika migahawa ambapo wameitaka idara ya afya  na usafi wa mazingira kutoa elimu kwa wamiliki wa migahawa, kuhusu madhara ya kuhifadhi vyakula vya moto katika mifuko ya plastiki, pia kuhakikisha kwamba vyakula wanavyowauzia wateja wao ni vyamoto, sambamba na kuwahudumia wateja katika hali ya usafi ,na kuweka mazingira ya migahawa yao katika hali ya usafi.

Naye Afisa lishe wa wilaya ya Kiteto bibi Beatrice Rutanjuka ametoa angalizo kuhusiana na bidhaa ambazo muda wake wa matumizi umekwisha, hapa Rutanjuka anasema “Mwaka umekwisha sasa, tumeingia mwaka mwingine, kuna bidhaa ambazo muda wake wa matumizi utakuwa umekwisha, lakini bado zinaendelea kuuzwa. Na kutokana na watanzania wengi kutokuwa na utamaduni wa kuangalia muda wa matumizi kabla ya kununua bidhaa, wataendelea kuzinunua na kuzitumia.Matumizi ya bidhaa hizo yanaweza kuwasababishia walaji kupata saratani. Ni vema idara ya afya na usafi wa mazingira ifanye ukaguzi wa kina ili bidhaa zilizoisha muda wake ziondolewe sokoni”.


Kadhalika Rutanjuka amezungumzia kuhusu matumizi ya chumvi , ambapo amewataka watu kutumie chumvi zenye madini joto.Amesisitiza kuwa hakuna mahali ambapo mtu anaweza kupata madini joto, zaidi ya kwenye chumvi,hivyo ni muhimu kwa idara ya afya na  wajumbe wote wa kamati ya lishe kuweka msisitizo katika kuelimisha jamii kutumia chumvi yenye madini joto.

Rutanjuka pia amezungumzia kuhusu chumvi zinazouzwa magulioni ambazo hazina madini joto, ambapo amesema kwamba ni vema idara ya afya ikafanya utafiti kufahamu upatikanaji wa chumvi hiyo ni wa kiasi gani,wasambazaji wake ni wakina nani ili taarifa sahihi kuhusu upatikanaji wa bidhaa hiyo zipatikane, zitumwe mkoani, Afisa lishe mkoa afanye utaratibu wa kuagiza madini joto, chumvi hiyo iwekewe madini hayo kabla haijasambazwa kwa wafanyabiashara warejareja na kuwafikia walaji.Kwani ni vizuri kutafuta suluhisho la tatizo, kwa kuiwekea madini joto chumvi hiyo kuliko kuzuia isiuzwe, hali ya kuwa chumvi hiyo imekuwa ikichimbwa ,na watu wameendelea kufanya biashara hiyo kwa miaka mingi.

Aidha baadhi ya wajumbe wamehoji kuhusu ubora wa mafuta ya alizeti ambayo yanakamuliwa na viwanda vidogo vidogo vilivyoko wilayani hapa,  usalama wa mafuta yanayouzwa na wanyabiashara wadogo, ambayo hupatikana baada ya kuchemsha mabaki ya alizeti iliyokwisha kukamuliwa viwandani maarufu kama tope na ladha ya uchungu ambayo wakati  mwingine husikika katika mafuta hayo.

Akijibu hoja za wajumbe kuhusu mafuta ya alizeti mwakilishi wa umoja wa viwanda vidogo vidogo vya kukamua alizeti ndugu Mohamed Ismail amesema kwamba mafuta yanayotokana na kuchemshwa kwa mabaki ya alizeti iliyokwisha kamuliwa sio salama kwa walaji. Kuhusu ladha ya uchungu kwenye mafuta Ismail amesema kwamba baadhi ya wakulima wa alizeti huvuna alizeti ikiwa haijakomaa vizuri, vilevile alizeti isipopepetwa vizuri, na ikakamuliwa ikiwa na pumba,pumba hizo husababisha mafuta kuwa na ladha ya uchungu.

Katika hatua nyingine kaimu afisa afya na usafi wa mazingira wilaya ya Kiteto ndugu Ezekieli Kimolo amesema kwamba baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakifanya biashara ya kukamua alizeti kiholea bila kujisajili hivyo wanapowatembelea kwa ajili ya ukaguzi hufunga na kukimbia.Vilevile amezungumizia kuhusu uhifadhi wa alizeti kabla ya kukamuliwa, ambapo amesema kwamba wafanyabiashara wengi huhifadhi mahali ambapo hakuna sehemu za kuingiza hewa, na wakati mwingine huhifadhi chini kwenye sakafu, jambo ambalo linasababisha alizeti kuharibika, hivyo kusababisha mafuta yanayokamuliwa kutokuwa na ubora na ladha inayotakiwa.

Hata hivyo Kimolo amesisitiza kwamba wamekuwa wakifuatilia na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara sio kwenye viwanda vya kukamua alizeti tu, bali kwa wafanyabiashara wote wa bidhaa za vyakula, na kwamba ufuatiliaji  wa karibu zaidi utaendelea ili kuendelea  kulinda afya za walaji.

Kikao hicho cha robo ya pili ya mwaka,kilikuwa na ajenda 8, moja wapo ya ajenda hizo ikiwa ni uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli za lishe  ambapo idara na vitengo mbalimbali vya Halmashauri vinavyohusika na  masuala ya lishe kama idara ya mifugo, idara ya kilimo,idara ya maji, idara ya mipango, idara ya elimu msingi, idara ya elimu sekondari,idara ya maendeleo ya jamii, idara ya afya na usafi wa mazingira,kitengo cha lishe, kitengo cha dawa na vifaa tiba, kitengo cha afya ya uzazi na mtoto, pamoja na taasisi mbalimbali kama Umoja wa Viwanda Vidogo Vidogo Kiteto, Baraza la  Waislamu (BAKWATA)-wilaya ya Kiteto,‘Mwanasatu Development Organization’ (MWADO) ziliwasilisha taarifa zake.Ajenda nyingine ilikuwa ni majadiliano kuhusu taarifa zilizowasilishwa pamoja na kuweka maazimio .





.........MWISHO..........

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUA: HATIMAYE KALOLENI YAPATA SHULE MPYA YA MSINGI

    July 30, 2025
  • SHULE YA MSINGI KINANGALI NAYO YANUFAIKA NA MRADI WA BOOST

    July 30, 2025
  • SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAENDELEA KUWEKEZA KWA VITENDO: KURASH YAPATA MRADI MWINGINE WA MILIONI 153 KUPITIA BOOST

    July 30, 2025
  • KATA YA BWAWANI YAPATA MRADI WA SHULE MPYA YA ELIMU MSINGI.

    July 28, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa