Kamati ya Lishe ya Wilaya ya Kiteto imefanya kikao chake cha utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha Robo ya Nne kwa mwaka 2024/25, kikao kilichofanyika tarehe 25 Julai 2025.
Kikao hicho kiliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Bi. Irene Mosha.
Wawakilishi kutoka idara mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, taasisi za serikali, madhebhebu ya dini mbalimbali pamoja na wadau wa utelekezaji wa afua za lishe, walishiriki kikao hicho kwa ajili ya kuwasilisha taarifa za utekelezaji, mafanikio na changamoto katika kutekeleza afua hizo katika robo iliyopita.
Wajumbe wa kamati hiyo kwa pamoja walipata fursa ya kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wadau hao na kutafuta suluhisho ili kuweza kufanya vizuri zaidi katika robo hii.
Katika kikao hicho Bi. Mosha alitoa wito wa kuwaweka pamoja wasindikaji wa vyakula vyote wilayani hapa ili kusaidia kuboresha umoja wao na kuongeza idadi ya wasindikaji kwenye kata zote 23.
Aidha Bi Mosha aliwataka washiriki wote kuendelea kushirikiana kwa karibu katika kutekeleza afua za lishe kwa kuzingatia vipaumbele vya wilaya na sera za taifa. Alisisitiza kuwa hali bora ya lishe ni msingi wa ustawi wa jamii na maendeleo ya Kiteto kwa ujumla.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa