Aprili - 2017, Kamati ya Ulinzi na Usalama Kiteto, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya (DC) Mh.Tumaini Magessa, wakiwa na mtuhumiwa Geoge Juma (50) mwenye shati la kijani akiwa na mwanae wa Pori Namba Mbili aliyetuhumiwa kulima, kutumia na kuuza zao haramu aina ya bangi huku akimiliki silaha aina ya bunduki kinyume cha sheria..
Bw, Geoge Juma (50) akiwa chini ya ulinzi wa Polisi Kiteto
Mkuu wa Polisi Kiteto, Fadhili Luoga katika jitahada ya kumtia nguvuni mhalifu..
Bangi ikiteketezwa Kiteto..
Mkulima huyo anafahamika kwa jina la Geoge Juma (50) mkazi wa maeneo ya pori namba mbili kijiji cha Kimana, Kata ya Partimbo,
ambapo baada ya kufikishwa Mahakamani, alikiri kulima, kutumia na kuuza bangi, huku akimiliki silaha aina ya bunduki kinyume cha sheria,
kisha hakimu kumhukumu miaka 35 kwenda jela kwa makosa hayo,
Kwa mujibu wa Mussa Mahakamani hapo alikiri kulima, kutumia na kuuza bangi, akisema hajashurutishwa katika maamuzi haya bali ni matakwa yake binafsi ingawa anajua Serikali inakataza..
Picha ni kwa hisani ya Mohamed Hamad, wa mwanganamatukio Kiteto
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa