Kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia inaendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii.Kampeni hii hufanyika kila mwaka kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 10, ikiwa ni kipindi maalumu cha kimataifa cha kuongeza uelewa na kuhamasisha hatua za kupinga ukatili wa kijinsia.Tarehe hizi zimeunganishwa kuanzia Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake (Novemba 25) hadi Siku ya Haki za Binadamu (Desemba 10), zikionyesha kuwa mapambano dhidi ya ukatili ni sehemu ya kulinda haki za binadamu.Wilayani Kiteto, kampeni hii inatekelezwa kwa njia ya kutoa elimu kupitia mikutano ya hadhara, semina na uhamasishaji katika makundi ya wanawake, wanaume, vijana na wanafunzi, ikiwa ni jitihada za kuongeza uelewa na kuzuia vitendo vya ukatili katika jamii.Kauli mbiu ya kampenji hii mwaka 2025, ni “TUUNGANE Kukomesha Ukatili wa Kijinsia Mitandaoni”

Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa