Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Mwema Emmanuel Julai 23,2025 ameongoza mkutano wa hadhara katika Kata ya Bwawani kwa lengo la kuutambulisha rasmi mradi mkubwa wa ujenzi wa shule mpya ya elimu msingi katika Kitongoji cha Mji Mpya.
Mradi huo una thamani ya shilingi milioni 330.7 na unatekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu kupitia programu ya BOOST ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha miundombinu ya Elimu Awali na Msingi na kuhakikisha mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia.
Ujenzi huo utahusisha miundombinu muhimu ya shule ikiwa ni pamoja na: Madarasa sita (06) ya elimu ya msingi, madarasa mawili 02) ya mfano kwa elimu ya awali, matundu ya vyoo sita (06) kwa wanafunzi wa elimu ya msingi na matundu sita(06) ya vyoo kwa wanafunzi wa awali.
Aidha, ujenzi huo utahusisha vyoo matundu mawili (02) kwa walimu pamoja na jengo moja la utawala.
Kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo mpya kunatarajiwa kutapunguza adha ya watoto kutembea umbali mrefu kutafuta elimu na kuongeza mahudhurio shuleni na pia utapunguza msongamano katika shule ya Msingi Bwawani.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa