Katika kuelekea kuupokea Mwenge wa Uhuru Wilayani Kiteto, Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Bi Karolina Mthapula, amefanya ziara kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ambayo inatarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru wilayani hapo.
Katika ziara hiyo ambayo imefanyika Septemba 30, 2023, Bi Mthapula aliongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Mratibu wa Mwenge Mkoa pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Bi Mthapula na msafara wake walikagua miradi miwili ambayo itazinduliwa na Mwenge wa Uhuru. Miradi hiyo ni Daraja la Orkine lililopo kata ya Songambele na mradi wa Maji uliopo Majengo Mapya katika kata ya Kaloleni.
Aidha Msafara huo ulikagua pia miradi miwili ambayo itafunguliwa na Mwenge wa Uhuru. Miradi hiyo ni vyumba viwili vya madarasa pamoja na ofisi katika Shule ya Msingi Esukuta iliyopo kata ya Dosisodi pamoja na ufunguzi wa Shule ya Msingi Azimio A, katika kata ya Matui iliyojengwa kwa leongo la kupunguza msongamano katika shule ya Msingi Azimio.
Vilevile Bi. Mthapula na Msafara wake walipita kukagua mradi wa ujenzi wa majengo matatu ya Hospitali ya Wilaya ambayo Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi huo.
Pamoja na hayo, Mwenge wa Uhuru wilayani Kiteto unatarajiwa kukagua mradi wa Mazingira Uliopo katika Shule ya Sekondari Nasa Matui pamoja na kufungua klabu ya Wapinga Rushwa shuleni hapo.
“Miradi ni mzuri kwakweli naomba nimpongeze Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, watumishi na watendaji wote kwa miradi hii. Kilichobaki sasa ni kuhakikisha nyaraka zote za miradi zinawekwa sawa na pia kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru”. Alisema Bi Mthapula.
Mkoani Manyara Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa Jumamosi Oktoba 7,2023 kupitia Wilaya ya Kiteto eneo la Dosidosi. Wilayani hapoa, ujumbe wa Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kutolewa katika Stendi ya Mabasi Engusero. Aidha mkesha wa Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Michezo wa Wilaya uliopo Kibaya kabla ya kukabidhiwa katika Wilaya ya Simanjiro siku ya Oktoba 8,2023 .
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa