Kikao cha Robo ya Tatu ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Kilichoanza Leo Tarehe 16.05.2017 Hadi Tarehe 17.05.2017
Imetumwa : May 16th, 2017
Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Lairumbe Mollel Akisoma Dua Kabla ya Kufungua Kikao.
Mkurugenzi Mtendaji (W) Bw. Tamim H. Kambona Akisalimia Wajumbe na Kumkaribisha Mh.Mwanyekiti Lairumbe Mollel
Waheshimiwa Madiwani (waliovaa majoho ya rangi ya Damu ya Mzee) Wakiwa Katika Kikao.
Wakuu wa Idara Wakifuatilia Kikao cha Baraza la Madiwani Kiteto
Ndipo Ilipofika Wakati wa Waheshimiwa Madiwani Kuwasilisha Taarifa za Miradi ya Maendeleo ya Kata Wanazotoka
kwa Kipindi cha Robo Mwaka ya Tatu (Januari - Machi 2017)
Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani Katika Uwasilisha wa Taarifa za Miradi ya Maendeleo ya Kata zao.
Kaimu Afisa Ardhi na Maliasili Wilaya Bw. Emmanuel Gulisha, Akitoa Ufafanuzi wa Kitaalamu kuhusu Ardhi katika Kikao
Afisa Mifugo na Uvuvi Wilaya Bw. William E. Msuya, Akitoa Ufafanuzi wa Kitaalamu Kuhusu Usajili wa Masoko ya Mifugo (Minada)
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Dr. G. Lupembe Akitoa Ufafanuzi wa Kitaalamu Katika Kikao
Ndipo Siku Iliyofuata Wenyeviti wa Kamati Mbalimbali Waliwasilisha Taarifa za ili Ziweze Kufanyiwa Kazi.
Mwenyekiti wa Kamati za Jamii Mh. Diwani kata ya Dosidosi, Benzi Hassan Akiwasilisha Taarifa ya Kamati hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati za Uchumi na Mazingira Mh. Diwani Paulo Tunyoni wa Kata ya Partimbo Akiwasilisha Taarifa Hiyo.
Mh. Diwani wa Kata ya Bwagamoyo (Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri) Akiwasilisha Taarifa hiyo ya Kamati ya Fedha na Mipango Kwaniaba ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
TAARIFA KAMILI...
Katika Baraza hilo, majadiliano mbalimbali ya kikao yalikuwa ni kutilia mkazo juu ya usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo ya wananchi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto. Ili kuleta matokeo chanya utaratibu wa namna ya kumpata Mkandarasi bora, ufuatiliaji na usimamizi wa uhakika katika kutekeleza mradi husika na ulipaji wa fedha kwa Mkandarasi kwa kufuata taratibu za kisheria ndiyo suluhisho. Hata hivyo katika miradi mingi iliyooekana kufanya vizuri zingatio la mambo matatu tajwa hapo juu ndiyo yaliyozingatiwa hadi kupata miradi iliyo bora na inaoendana na thamani ya fedha iliyolipwa.
Uwasilishaji wa Taarifa za Kata Januari - Machi 2017.
Katika mawasilisho mbalimbali ya Waheshimiwa Madiwani takwimu zinaonyesha kuna idadi kubwa ya wananchi wanaojiunga na Bima ya Afya ya Jamii ijulikanayo kama “Mfuko wa Afya ya Jamii Ulioboreshwa” ( iCHF ) ambapo lengo ni kila mwananchi kupata huduma ya Afya popote katika Hospitali za Serikali na baadhi ya Hospitali Binafsi zilizoidhinishwa kwa gharama ndogo kwa mwaka mzima kwa kuchangia kiasi cha Shilingi (T) 30,000/=. Kwa Kata 23 za Halmashauri ni safu ya watu kati ya 100 hadi 250 kwa makusanyo ya takribani milioni 3 hadi milioni 7 kwa kila Kata katika kipindi cha Januari hadi Machi 2017, katika hili Waheshimiwa Madiwani wamefanya hamasa kubwa kwa wananchi katika Kata zao.
Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto Bw. Tamim Kambona akifafanua jambo kuhusu miradi katika Kikao cha Baraza hilo
Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto amesema hatamvumilia Mzabuni wala Mtumishi yeyote ambaye ataenda kinyume na utaratibu wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya wananchi kuanzia upatikanaji wa vifaa vyenye vigezo vilivyowekwa, kununuliwa vifaa husika kwa wakati uliokubalika, kuwepo vifaa husika katika eneo la mradi, kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kisha timu maalumu kujiridhisha kwanza kabla ya malipo kutolewa lakini pia kuhakikisha kwamba kama ni malipo ya vibarua basi yawafikie walengwa; utaratibu huu ndiyo uliosaidia Halmashauri kupata miradi mizuri na unaendelea kutumika katika utekelezaji wa miradi inayoendelea na miradi mipya itakayofuta ya mwaka 2017/2018.
Afisa Utumishi Wilaya Bw. Raphael Makoninde Akiwasilisha Taarifa Maalumu Kuhusu UHAKIKI wa Watumishi
kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto na Maagizo Rasmi ya Kitaifa Juu ya Zoezi Hilo.
Uwasilishaji wa Taarifa za Uhakiki wa Watumishi wa Serikali
Watumishi 1476 Walihakikiwa Vyeti vya Kuhitimu Kidato cha IV na VI na Vyeti vya Taaluma kwa Walimu Kati Yao Watumishi 1383 Walikuwa na Vyeti Halali, Watumishi 66 Vyeti vya Kugushi, Watumishi 5 Vyeti Vyenye Utata na Watumishi 22 walikuwa na vyeti Visivyokamilika (incomplete).
Hata Hivyo Maagizo Kuhusu Uhakiki Huu kwa Watumishi wa Serikali ni Haya Yafuatayo :-
kuwaondoa watumishi wote waliogushi vyeti kwenye orodha ya malipo ya mishahara na kuwaandikia barua ya kuwaachisha kazi
kuwaondoa watumishi wote wenye vyeti vya utata kwenye orodha ya malipo ya mishahara na kuwasilisha umiliki wa vyeti vyao Balaza la Mitihani Tanzania kabla ya tarehe 15.05.2017
kuwajulisha watumishi wote wenye vyeti pungufu kuwasilisha vyeti vyao Balaza la Mitihati Tanzania kabla ya tarehe 15.05.2017 kwa ajili ya kuhakikiwa upya
watumishi wanaokata rufaa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora wafanye hivyo kabla ya Tarehe 15.05.2017
Mkurugenzi Mtendaji (W) Bw. Tamim Kambona alipongezwa kwa kuwa mstari wa mbele katika kuifutatilia miradi yote kwa kujiridhisha katika ukaguzi yeye mwenyewe.
Pia Baraza la Madiwani liliipongeza Kamati ya ulinzi na usalama inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh.Tumaini Magessa kwa kuimarisha usalama Wilayani kwetu Kiteto kwani hadi sasa wakulima, wafugaji na wafanyabiashara mbalimbali na wananchi kwa ujumla wao wanaendelea na shuguli zao za kila siku bila shida.
Hitimisho.
Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Lairumbe Mollel akiahirisha Kikao cha Baraza la Madiwani tarehe 17.05.2017
Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri Kiteto Lairumbe Mollel alisisitiza kwamba hakuna mgogoro wa wakulima na wafugaji Wilayani Kiteto kwani kuko shwari na watu wote waendelee kufanya shughuli zao kama kawaida. Pia aliongeza kuwa Watumishi na Madiwani ni muhimu kushirikiana na kufanya kazi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni zilizowekwa kwani hatutasita kumchukulia hatua yeyote atakayebainika kukwamisha shughuli za maendeleo katika Halmashauri anayoisimamia yeye.