Wataalamu kutoka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) wakiongozwa na Mkurugenzi wake, Ndg. Asangye Bangu, Agosti 28,2025, wametembelea Wilayani hapa kwa lengo la kukagua utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi za ghala kwa zao la mbaazi.
Katika ziara hiyo, ujumbe wa WRRB ulipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Remidius Mwema Emmanuel, ambapo walifanya kikao cha pamoja na uongozi wa wilaya akiwemo Katibu Tawala Ndg. Mufandii Msaghaa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri CPA. Hawa Abdul Hassan pamoja na wataalamu kutoka ofisi yake.
Aidha, wageni hao walitembelea na kukagua ghala jipya la Halmashauri lililojengwa kwa mapato ya ndani, ambapo walieleza kufurahishwa na uwekezaji huo mkubwa uliofanywa na halmashauri kupitia mapato ya ndani. Uwekezaji huo unatarajiwa kuongeza ufanisi katika uhifadhi na usimamizi wa mazao haswa mbaazi ambazo zinauzwa kupitia mfumonwa stakabadhi za ghala.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa