Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Yapata Hati Safi na Kukusanya Zaidi ya Bilioni 1.9 kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017, Haya Yamejiri leo Kwenye Kikao Maalumu cha Balaza la Madiwani Kilichofanyika Kwenye Ukumbi wa Halmashauri (W) Leo Tarehe 30.06.2017
Imetumwa : June 30th, 2017
Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Lairumbe Mollel (wa kushoto) Akisoma Dua Maalumu Wakati wa Kufungua Kikao hiyo.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim H. Kambona.
Mtunza Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Nassoro Mkwanda Akiwasilisha Hoja Katika Kikao.
Waheshimiwa Madiwani Wakisoma Taarifa Mbalimbali za Kikao.
Wakuu wa Idara na Vitengo Katika Kikao
Mh. Diwani wa Kata ya Lengatei Mainge Lemalai Akichangia Hoja Katika Kikao.
Mh. Diwani wa Kata ya Kaloleni Christopher Parmet Akichangia Hoja Katika Kikao.
Mh. Diwani wa Kata ya Partimbo Paul Tunyoni Akichangia Hoja Katika Kikao.
Mh. Diwani wa Kata ya Dosidosi, Benzi Akichangia Hoja Katika Kikao
Mh.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Lairumbe Mollel Akihitimisha Kikao.
Wajumbe walifahamishwa na Mtunza Hazina wa Wilaya kuwa Halmashauri imepata Hati Safi kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. Hata hivyo mapato ya makusanyo ya ndani kwa Halmashauri yamepanda kutoka Shilingi milioni mia nane sabini (Tsh. 870,000,000.00) ambayo ni sawa na 78% kwa mwaka wa fedha 2015/2016 hadi kufikia zaidi ya Shilingi bilioni moja mia tisa milioni (TSh. 1,900,000,000.00) sawa na 93% ya mapato ya Makusanyo ya ndani kwa Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Kufikia lengo hili ilikuwa si kazi ndogo bali ni jitihada za Mkurugenzi wa Halmashauri (W) Kiteto Bw. Tamim H. Kambona kwa utendaji wake unaoendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano, uongozi mzima wa Halmashauri, Waheshimiwa Madiwani, Wataalamu,Mkuu wa Wilaya na Wadau wetu wakubwa ambao ni wananchi, kwani imesaidia kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuboresha na baadhi ya huduma mbalimbali na kuondoa kero kwa wananchi hususani katika Afya, Maji na Elimu.
Hata hivyo Mh. Mwenyekiti alisisitiza kuwa tunapaswa tujipange vizuri kwa mwaka huu kwani mvua ilikuwa ya wastani na kwa maeneo kadhaa tu lakini tuongeze bidii kwa ukusanyaji wa machine za kielektroniki (POS) ili tuongeze uwezo wakutatua kero za wananchi wa Wilaya ya Kiteto na kupiga vita umaskini.