Shirika lisilo la kiserikali KINNAPA limekadhi Mradi wa Ufundi Ushonaji kwa Sekondari ya Sunya ili kuuendesha.
Hafla ya makabidhiano ya mradi huo imefanyika Julai 31,2024, katika Shule ya Sekondari Sunya na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wananchi, viongozi wa Chama na serikali na wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Kiteto. Mgeni Rasmi wa hafla hiyo alikua Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Remidius Mwema.
KINNAPA imekua ikifanya jitihada ya kuwasaidia wanafunzi waliokatisha masomo kurudi shuleni ili kuendelea na masomo ila ilikuja kubaini kua sio wanafunzi wote wapo tayari kurudi shuleni kuendelea na masomo ya kawaida darasani bali wapo ambao wanahitaji kujifunza ufundi.
Baada ya kutambua hilo, KINNAPA iliamua kuongeza mkondo wa ufundi katika shule ya Sekondari Sunya ili kuwapa fursa wanafunzi waliokatiza masomo kupata ujuzi.
Mradi huo wa ufundi umegharimu kiasi cha fedha 5,100,000 ambayo imetumika kununua mashine(cherehani) mbalimbali tano ikiwemo mashine za kushonea na kudarizi, kununua vifaa vyote vya ushonaji, kununua majora ya vitambaa vya sare za shule ambayo yanatumika kama mtaji wa kuwezesha kuendeleza mradi huo. Aidha sehemu ya fedha hizo ilitumika kuwasaidia nauli wanafunzi wa darasa hilo la ufundi.
Mbali na hayo, KINNAPA pia imesaidia upatikanaji wa mwalimu wa ufundi kwa darasa hilo ambapo uongozi wa shule unapaswa kuwajibika kumlipa mwalimu huyo mshahara. Hii imepelekea Mkuu wa Wilaya Mhe. Mwema kutoa kiasi cha fedha 300,000 ili kuisaidia shule hiyo mshahara wa mwalimu huyo na pia shirika la SULEDO limeahidi kutoa pia 300,000 lengo hilohilo.
Mradi huo ambao kwa sasa una wanafunzi 13, umekadhibiwa kwa Mkuu wa Sekondari ya Sunya ili kuuendesha na mafunzo hayatatolewa kwa wanafunzi waliokatiza tu masomo bali hata kwa wanafunzi wengine watakaohitaji kupata ujuzi huo.
Akijibu swali ambalo liliuliza kwanini mradi huo umetekelezwa Sunya na sio kwenye kata nyingine, Mratibu wa KINNAPA Kiteto Ndg. Abrahamu AKilimali, amesema kwamba Sunya ndio walianza kuonesha muitikio wa kuwarudisha shuleni wanafunzi waliokatisha masomo na vilevile Sunya ina idadi kubwa ya watoto waliorudi kuendelea na masomo baada ya kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa