Jengo la upasuaji kama linavyoonekana katika picha.
Wilaya ya Kiteto iko mbioni kuwa na kituo cha afya cha kisasa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa majengo matano , ambayo yanajengwa katika kituo cha afya Sunya.
Ujenzi huo ambao ni wa kihistoria katika wilaya ya Kiteto,unatarajiwa kukifanya kituo cha afya Sunya kuwa cha kisasa ambapo majengo matano yamejengwa, yakiwa ni jengo la maabara, jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti ,nyumba ya mtumishi pamoja na wodi ya mama na mtoto .
Nyumba ya mtumishi kama inavyoonekana katika picha.
Jengo la maabara kama linavyoonekana katika picha.
Jengo la kuhifadhia maiti kama linavyoonekana katika picha
Jengo la wodi ya mama na mtoto kama linavyoonekana katika picha
Ujenzi huo ulioanza rasmi mwanzoni mwa mwezi Januari, 2018, ulisimamishwa Januari 10, 2018 baada ya ramani za majengo ya; upasuaji, wodi ya mama na mtoto pamoja na jengo la kuhifadhia maiti kuwa tofauti na ambavyo zilitakiwa kuwa.Hata hivyo mwanzoni mwa mwezi wa tatu ujenzi uliruhusiwa baada ya kupatikana kwa ramani sahihi.
Majengo hayo ambayo manne kati ya matano yameshapauliwa, yanatarajiwa kukabidhiwa kwa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ifikapo Mei 31, 2018 yakiwa yamekamilika.Hadi sasa ujenzi huo umegharimu fedha za Kitanzania sh. 137,396,342/=.Ambapo serikali ilikiasi cha shilingi za kitanzania milioni 400 kwa kituo cha afya cha Sunya kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo , pamoja na ujenzi wa kichomea taka, ambacho kitajengwa mara baada ya majengo yote matano kukamilika.ikiwa ni katika mkakati wa serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya ili kuwaondolea wananchi wake kero ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.
............... MWISHO...............
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa