• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Kiteto Yazindua Utoaji Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi

Imetumwa : April 30th, 2018

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa akizindua utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.Uzinduzi huo umefanyika  katika hospitali ya wilaya.

Muuguzi akifanya matayarisho ili kutoa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ,katika uzinduzi wa chanjo hiyo  uliofanyika   katika hospitali ya wilaya ya Kiteto.


Muuguzi akiwapa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi  wanafunzi waliofika katika hospitali ya wilaya kwa ajili ya kupata chanjo hiyo katika uzinduzi  uliofanyika  katika hospitali ya wilaya ya Kiteto.


Muuguzi akiwaelekeza  wanafunzi  kuhusu utaratibu wa kupata chanjo ya pili ya saratani ya mlango wa kizazi, baada ya kuwapa chanjo ya kwanza , katika uzinduzi wa chanjo hiyo  uliofanyika  hospitali ya wilaya ya Kiteto.


Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini  Magessa akifuatilia  kuhakikisha kwamba wanafunzi waliopewa chanjo, wameelewa vizuri kuhusu utaratibu wa kupata chanjo ya pili ya saratani ya mlango wa kizazi, katika uzinduzi wa chanjo hiyo  uliofanyika  hospitali ya wilaya ya Kiteto.


Wanafunzi pamoja na mwalimu wao wakisubiri kupewa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi,wakati wa uzinduzi wa utoaji chanjo hiyo uliofanyika katika hospitali ya wilaya ya Kiteto.


Viongozi wa dini, viongozi  wa mila ,watendaji kata, pamoja wakazi mbalimbali wa wilaya ya Kiteto, wakiwa katika  uzinduzi wa utoaji chanjo  ya  saratani ya mlango wa kizazi  uliofanyika katika hospitali ya wilaya ya Kiteto.



.......................HABARI KAMILI .................



Wilaya ya Kiteto  imezindua chanjo ya saratani ya mlango wa Kizazi.Uzinduzi huo umefanywa  leo na mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa katika hospitali ya wilaya .


Mhe. Tumaini Magessa amesema kwamba watoto   wanahitaji kukingwa na saratani ya mlango wa kizazi, kwani jamii imekuwa ikiangamia kutokana na saratani hiyo.Akizungumza na wanafunzi wa kike waliofika kwa ajili ya kupata chanjo, Mhe. Magessa amewataka  kutojiingiza katika kufanya mapenzi katika umri mdogo, Mhe. Magessa amesema “Mimba za utotoni ni tatizo kwenye hili,kuanza matendo ya watu wazima katika umri mdogo ni tatizo kwenye hili . Mtu asikudanganye ana bodaboda, kwamba mimi nitakuwa nakupeleka pale kaloleni shule ya msingi basi ukajua ni ofa, ukafika mahali ukajiingiza kwenye matendo ambayo ni ya watu wazima usikubali, ukikubali maana yake  umejiingiza kwenye hatari ya kupata hili tatizo’’.


Akisisitiza  kuhusu umuhimu wa wanafunzi  hao kutokujihusisha na masuala ya kujamiiana,Mhe Magessa amesema “serikali imetoa kinga hii ,kuwa na kinga isiwe sababu ya kusema kwamba mimi sasa nimesha kingwa  kwa hiyo sasa ni mwendo mdundo, utakutana na jingine tena mbele ya safari.Serikali imechukua jitihada hii ya kuwakinga,na ninyi mchukue jitihada ya kusema No. Kazi yenu ni rahisi sana,mjifunze kusema No.Sio kwa sababu serikali imewapa chajo,ndio mkimbilie kufanya matendo ya watu wazima”.


Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mhe. Lairumbe Mollel amesema kwamba saratani ya mlango ya Kizazi  imekuwa ni shida kwa kina mama,na kwamba ili kuidhibiti isiendelee  kuwa sababu ya vifo kwa kina mama, ni vema wananchi wote wa wilaya ya Kiteto wenye watoto wa kike wa umri wa miaka 14  kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya ili kupata chanjo. Akisisitiza juu ya elimu ya saratani ya mlango wa kizazi na chanjo hiyo kuwafikia watu katika maeneo yote wilayani Kiteto, mhe. Mollel amesema ‘‘walimu,watendaji ,wakazi wa Kiteto pamoja na viongozi wetu wa mila nimewaona hapa.msambaze elimu hii vijijini na katika maeneo yote,ili watoto wote wa umri wa miaka 14 wapate  chanjo hii.Ninawaomba sana ndugu zangu hii elimu itapakae kote.Ukiambiwa shida ya huu ugonjwa ni nini, unatamani hata mtoto wa mwaka mmoja achanjwe’’.


Uzinduzi huo ulitanguliwa na kikao cha Huduma ya Afya ya Msingi ( PHC), ambapo ajenda kubwa ya kikao hicho ilikuwa ni ushirikishaji na utoaji hamasa juu ya utoaji chanjo ya saratani ya mlango ya kizazi kwa viongozi wa dini,viongozi wa mila pamoja na wazee maarufu , lengo likiwa ni kusaidia kuhamasisha jamii katika nyumba za ibada na maeneo wanayoishi. Katika kikao hicho Mganga mkuu wa wilaya ya Kiteto Daktari Malkiadi Paschal Mbota ametoa elimu kuhusu saratani ya mlango wa kizazi ambapo amesema kwamba mimba za utotoni, kuanza kushiriki tendo la kujamiiana katika umri mdogo na kushiriki tendo la kujamiiana na wapenzi wengi ni  miongoni mwa visababishi vya  maambukizi ya virushi vya HPV ambavyo husababisha saratani ya mlango wa Kizazi. Aidha Dkt. Mbota amewataka wajumbe wa kikao hicho kuhamasisha jamii kupeleka watoto kupata chanjo ili kuwa na  kinga dhidi ya ugonjwa huo,sambamba na kuhuibiri jamii kubadili tabia na kuwa waaminifu katika mahusiano ya kimapenzi ili kuepuka maambukizi ya virusi vinavyosababisha saratani ya mlango wa kizazi.

Mganga mkuu wa wilaya ya Kiteto  Dkt . Malkiadi Mbota akimkaribisha Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa kufungua kikao cha Afya ya Msingi (PHC) kuhusu utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi. Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa halmashauri . Aliyekaa upande wake wa kulia  ni kaimu katibu tawala wa wilaya Ndg. Fadhili Alexander.


Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa akifungua  kikao cha Huduma ya Afya ya Msingi (PHC)  kuhusu utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi. Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa halmashauri .Aliyekaa  upande wake wa kulia ni Mganga mkuu wa wilaya Dkt. Malkiadi Mbota, upande wake wa kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Ndg. Tamim Kambona.

Wajumbe wa  kikao cha Huduma ya Afya ya Msingi (PHC)  wakiendelea na kikao kuhusu utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi. Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa halmashauri .




..................... MWISHO.....................



Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa