• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Kiteto Yapongezwa Kupata Hati Safi

Imetumwa : July 21st, 2018

Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Manyara  Ndg. Anold Msuya akizungumza katika baraza maalumu la kujadili hoja za ukaguzi kwa mwaka 2016/2017.Baraza hilo limefanyika ndani ya ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto.

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa  akimkaribisha mwakilishi wa mkuu wa mkoa kuzungumza katika baraza maalumu la kujadili hoja za ukaguzi kwa mwaka 2016/2017.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mhe. Lairumbe Mollel akizungumza katika baraza maalumu la kujadili hoja za ukaguzi kwa mwaka 2016/2017.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto Ndg. Tamim Kambona  akizungumza katika baraza maalumu la kujadili hoja za ukaguzi kwa mwaka 2016/2017.



Mbunge wa jimbo la Kiteto Mhe. Emmanuel Papian akizungumza katika baraza maalumu la kujadili hoja za ukaguzi kwa mwaka 2016/2017.

Wahe. Madiwani pamoja na wakuu wa idara na vitengo  vya halmashauri wakiwa katika baraza maalumu la kujadili hoja za ukaguzi kwa mwaka 2016/2017.



.....HABARI KAMILI......




Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti ametoa pongezi kwa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa kupata hati safi katika ukaguzi mwaka 2016/2017.Pongezi hizo zimetolewa na mwakilishi wake ambaye pia ni afisa elimu wa mkoa wa Manyara ndugu Anold Msuya wakati wa kikao cha baraza maalum la madiwani la kujadili hoja za ukaguzi kwa mwaka 2016/2017 lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri mapema jana.

Katika hotuba yake iliyosomwa na mwakilishi wake Mhe. Mnyeti  amesema kwamba pamoja na kupata hati safi, baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kiteto lisimamie kwa ukamilifu kuhakikisha kwamba maeneo yaliyotajwa kuwa na udhaifu na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka 2016/2017 yanafanyiwa kazi kikamilifu,ikiwemo kujibu hoja za miaka ya nyuma , pamoja na maagizo ya kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali.

Aidha Mhe. Mnyeti amesema  kwamba Kila mkuu wa idara na kitengo atalazima kuwajibika na kushiriki kikamilifu wakati wa ukaguzi,tofauti na utaratibu ambao umekuwepo miaka ya nyuma ambapo jukumu la kujibu hoja za ukaguzi liliachwa kwa mweka hazina pamoja na watendaji wake wa idara ya fedha na mkaguzi wa ndani.

Mhe Mnyeti amesisitiza kuwa katika utaratibu wa sasa, atakaepaswa kujibu hoja za ukaguzi ni mkuu wa idara au kitengo kilichohusika  kuzalisha hoja . Na kwamba wakuu wa idara na vitengo watawajibika kuhangaika ili kuzuia hoja zisitokee, na pale zitakapokuwa zimetokea, watawajibika kutafuta majibu ya hoja hizo.Na kwamba wakuu wa idara na vitengo wanapaswa kuwajibika kikamilifu kuhakikisha kwamba  idara na vitengo vyao havizalishi hoja, na endapo zitazaliwa hoja, wakuu wa idara na vitengo vilivyozalisha hoja hizo watawajibishwa.


Kadhalika Mhe Mnyeti amelipongeza baraza la madiwani kwa usimamizi mzuri, na kuwataka Wahe. madiwani  kuhakikisha kwamba wanaendelea kusimamia  nidhamu ya matumizi ya fedha , ili Halmashauri yao iendelee kupata hati safi.

Katika hatua nyingine mwakilishi huyo wa mkuu wa mkoa ametoa pongezi kwa waheshimiwa madiwani pamoja na watendaji wote wa Halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji ndugu Tamim Kambona kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo.Akitoa pongezi hizo ndugu Msuya  amesema,“ Jana  nilifanikiwa kutembelea miradi yenu, nimejionea jinsi ambavyo miradi yenu mnayoitekeleza ilivyo katika viwango vya juu kabisa. Miradi inatekelezwa kwa kasi na kwa ubora unaotakiwa.Kama kuna jambo  Kiteto la kujivunia, ni kuwa na baraza makini kama hili, na kuwa na Mkurugenzi anayesimamia watendaji wakafanya kazi kwa ubora na kwa uadilifu mkubwa namna hii”.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini  Magessa  ametoa rai kwa watendaji wote ambapo amesema kwamba kwa sababu Halmashauri imepata hati safi, wanatakiwa kuwa makini katika utendaji ili kuzuia kuwepo kwa hoja nyingine . Akisisitiza kuhusu umakini katika utendaji Mhe. Magessa anasema “ Tusipokuwa makini maana yake ni kwamba tutaendelea kuacumulate hoja, wakati tayari zimeanza kufutwa, kwa hiyo tutegemee kabisa  kwamba hatuwezi kuacumulate tena hoja zingine.Wakaguzi wako hapa. Mara nyingi hoja hizi zinakuja kwa sababu ya kutokuwa na utii, yaani unafanya mambo nje ya kanuni,kwa hiyo kufanya mambo kwa kutokufuata kanuni ndiko kunasababisha  hizi hoja tunazoziona”.

Mhe Magessa   amewataka watendaji wote kuhakikisha kwamba wanafuata kanuni katika utendaji wao ili wasiendelee kuzalisha hoja nyingine. Akisisitiza kuhusu kauli yake hiyo Mhe Magessa amesema “Kama Halmashauri ni vizuri tukaelezana kwamba kila mmoja katika nafasi yake afuate kanuni.Kanuni ya serikali inasema nini fanya hicho, inaposhindikana kabisa basi tufuate utaratibu mwingine ambao tunaweza kuomba kufanya jambo fulani pasipo kuiingiza Halmashauri kwenye hoja’’.

Baraza maalumu la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kiteto limekaa ijumaa  kwa lengo la kujadili hoja za mkaguzi  wa hesabu za serikali kwa mwaka 2016/2017.  Jumla ya hoja Hoja 151, ziliibuliwa katika ukaguzi huo. Kati ya hoja hizo 151, hoja 101 ni za miaka ya nyuma, ambapo hoja  92 zimefungwa .Hoja za  mwaka unaoishia Juni 2017 ni hoja 50 , kati ya hoja hizo 50, hoja 32 zimefungwa.




........MWISHO.........

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUA: HATIMAYE KALOLENI YAPATA SHULE MPYA YA MSINGI

    July 30, 2025
  • SHULE YA MSINGI KINANGALI NAYO YANUFAIKA NA MRADI WA BOOST

    July 30, 2025
  • SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAENDELEA KUWEKEZA KWA VITENDO: KURASH YAPATA MRADI MWINGINE WA MILIONI 153 KUPITIA BOOST

    July 30, 2025
  • KATA YA BWAWANI YAPATA MRADI WA SHULE MPYA YA ELIMU MSINGI.

    July 28, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa