• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wanafunzi Kiteto Watakiwa Kuwa na Utayari Kubadilisha Matokeo

Imetumwa : August 3rd, 2018

Mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya juma la elimu ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Kiteto  Mhe. Tumaini Magessa akihutubia wakati wa maadhimisho hayo,ambayo kiwilaya yamefanyika  katika viwanja vya shule ya sekondari Kibaya.

Kaimu Mkurugenzi  ambaye pia ni Afisa Elimu Msingi (W) Mwl. Emmanuel Mwagala akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya juma la elimu wilayani kiteto.

 

Walimu ,wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali wa elimu wakiwa katika maandamano ya kilele cha maadhimisho ya juma la elimu wilayani Kiteto.

Mgeni rasmi na ujumbe wake alioambatana nao wakiwa katika vyumba  vya maonyesho kuhusu mada  mbalimbali za masomo,huku wanafunzi wakionyesha umahiri mkubwa katka kutoa maelezo kuhusiana na mada hizo.

Wanafunzi wakiimba wimbo katika kilele cha maadhimisho ya juma la elimu wilayani Kiteto.Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Kibaya mwishoni mwa juma.

Walimu , wanafunzi,wazazi pamoja na wadau mbalimbali wa elimu  wakiwa wamekusanyika katika kilele cha maadhimisho ya juma la elimu wilayani Kiteto.Maadhimisho hayo yamefanyika katika shule ya sekondari Kibaya mwishoni mwa juma.




.....HABARI KAMILI......




Mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya juma la elimu , ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Kiteto Mheshimiwa Tumaini Magessa amewataka wanafunzi kuwa na utayari wa kusoma kwa bidii ili waweze kuwa na maendeleo  mazuri kielimu na kupata matokeo mazuri katika mitihani . Mhe. Magessa ameyasema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya juma la elimu, ambayo kiwilaya yamefanyika katika shule ya sekondari Kibaya mwishoni mwa juma.

Akizungumza wakati wa hotuba yake, Mhe Magessa ameweka mkazo katika uwajibikaji wa pamoja,kwa walimu na wanafunzi ,kwamba wote wanawajibu wa kutimiza ili kupata matokeo mazuri katika elimu. Hapa Mhe. Magessa anasema “ Sisi viongozi tunatarajia mambo makubwa kutoka kwenu ,msituangushe. Wanafunzi wekeni bidii katika kusoma kwa hiyari yenu, hiyari  ndio inayoweza kubadilisha matokeo ya wilaya yetu.Kwa sababu hata kama walimu wakifundisha kwa bidii, kama wanafunzi hamjahiyari  kufanya vizuri,haiwezi kuleta matokeo mazuri”.

Kadhalika Mhe Magessa amewapongeza walimu kwa juhudi wanazozifanya katika kuboresha elimu ,ambapo amesema kwamba serikali itawalipa kwa juhudi hizo.Huku akiwataka wanafunzi kutojihusisha katika mambo ambayo yatawasababisha kutokuzingatia masomo yao.Akisisitiza kuhusu hilo Mhe. Magessa anasema “Nimesikia kwamba kuna wanafunzi wanaokesha disko siku za mwisho wa wiki.Tutawakamata na tutawashughulikia.Mwanafunzi uliyeko hapa tunakutegemea utoe matokeo mazuri kwenye elimu.Achana na mambo mengine, shughulika na elimu. Kazi ya wanafunzi iwe moja tu kusoma,na walimu wafundishe tupate matokeo”.

Aidha Mhe. Magessa ameeleza mikakati yake ya kuhakikisha kwamba Kiteto inafanya vizuri kwenye elimu, ambapo mikakati hiyo ni kutembelea shule zote kukagua namna ya ufundishaji kwa kuingia darasani kuuliza maswali yanayohusiana na masomo yanayofundishwa ili kuhakikisha  kama wanafunzi wanaelewa wanachofundishwa , kuzungumza na wazazi kuhusu namna ya kuweka utaratibu ili wanafunzi waweze kupata kifungua kinywa na chakula cha mchana shuleni, ambapo katika kufanikisha hili amewata wakuu wa shule zote kuandaa siku ya wazazi kuja shule yaani ‘parents day’ na yeye aalikwe ili kwa pamoja waweze kuzungumzia suala hilo ,pamoja na masuala mbalimbali yatakayosaidia kuinua kiwango cha taaluma .

 Mkakati mwingine ni kufanya jitihada za kupata walimu wa masomo ya sayansi pamoja na masomo mengine ambayo hayana walimu kwa kuwatumia walimu wa masomo hayo wanaofundisha katika shule za jirani  ndani ya wilaya .

Katika hatua nyingine zawadi mbalimbali zimetolewa na kukabidhiwa kwa wahusika na Mgeni rasmi Mhe Magessa ambapo shule zilizofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2017 zimezawadiwa , Shule ya Sekondari Ecco na shule ya msingi Laalakiri kila moja ikipewa shilingi 1,000,000, shule ya sekondari Lesoiti na shule ya msingi Sunya kila moja ikipewa shilingi 700,000 , shule ya sekondari Engusero na shule ya msingi Kibaya kila moja ikipewa shilingi  500,000.

Vilevile shule 12, 4 zikiwa za sekondari na 8 za msingi zilizoshiriki katika kuandaa maonyesho mbalimbali kwa ajili ya maadhimisho ya juma la elimu  zimezawadiwa kiasi cha shilingi 20,000 kila moja .Pia wanamichezo waliowakilisha wilaya katika UMISETA ngazi ya taifa na kufanya vizuri katika michezo mbalimbali nao wametunukiwa  vyeti vya pongezi,  .

 Juma la elimu huadhimishwa kila mwaka, ambapo kwa mwaka 2018 Kauli mbiu inasema “Uwajibikaji wa  Pamoja Katika Kutoa Elimu Bora”.



..........MWISHO.........

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUA: HATIMAYE KALOLENI YAPATA SHULE MPYA YA MSINGI

    July 30, 2025
  • SHULE YA MSINGI KINANGALI NAYO YANUFAIKA NA MRADI WA BOOST

    July 30, 2025
  • SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAENDELEA KUWEKEZA KWA VITENDO: KURASH YAPATA MRADI MWINGINE WA MILIONI 153 KUPITIA BOOST

    July 30, 2025
  • KATA YA BWAWANI YAPATA MRADI WA SHULE MPYA YA ELIMU MSINGI.

    July 28, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa