Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ipo katika maandalizi kuanzisha mradi wa ufugaji wa sungura katika shule za msingi sekondari wilayani hapa.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo Lishe Wilayani hapa, Ndg. Beatrice Lutanjuka, kwenye Kikao cha Robo ya Tatu cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Wilaya Aprili 16,2025.
Lutanjuka amesema kwamba lengo la mradi huo ni kuongeza ulaji vyakula vyenye asili ya wanyama, kwa wanafunzi na jamii pamoja na kuwajengea wanafunzi uwezo au maarifa ya ufugaji, ambapo pia wataweza kwenda kupeleka ujuzi huo kwenye kaya zao na hivyo jamii kupata muamko wa ufugaji na ulaji wa vyakula vyenye asili ya wanyama.
Aidha aliongeza kwa kusema kwamba, lengo la mradi ni kuzifikia shule zote 127 zilizopo wilayani hapa ila wameanza na shule nane ambapo shule hizo wameshajenga mabanda kwaajili ya ufugaji wa sungura hao na kwa sasa wanasubiria wataalam wa mifugo kwenda kukagua mabanda hayo kabla Kitengo hakija wapelekea mbegu hizo za sungura ili waanze ufugaji.
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto, Ndg. Mufandii Msaghaa, amekipongeza Kitengo cha Lishe na Ofisi ya Mkurugenzi kwa ujumla kwa jitihada hizo za mradi wa nyama kwenye shule.
Ndugu Msaghaa amesisitiza kuhakikisha kua mradi huo unafikia shule zote wilayani hapa haswa sekondari za bweni kwani wanafunzi wa kutwa wakikosa chakula kitokanacho na wanyama shuleni, wakirudi nyumbani wanaweza kukipata.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa