• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Kiteto yafanya kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya

Imetumwa : November 2nd, 2017

                                         Katibu tawala wa wilaya ya Kiteto ndugu Stephano Ndaki akiwatambulisha wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya

                                                                                              

Wajumbe wa kikao cha  kamati ya ushauri ya wilaya  wakifuatilia kwa makini taarifa mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika kikao hicho  

Mweka hazina wa wilaya ya Kiteto ndugu Nassoro Mkwanda akiwasilisha taarifa ya mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya ya Kiteto ya kuanzia mwezi Julai -  Septemba   2017

Kaimu afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto  ndugu Edga Kavenuke akiwasilisha taarifa ya bajeti  ya hamashauri ya wilaya ya Kiteto kwa mwaka 2017/2018 na taarifa ya utekelezaji wa miradi kwa mwaka 2016/2017

                                                                                                            

                Meneja wa TRA wilaya ya Kiteto ndugu Willjones Kisamba akiwasilisha taarifa ya mapato ya serikali kuu kwaka 2016/2017.

                                                                                                                             

                                                                                                                                                                                                                                                     

Wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya wakishauri  juu ya taarifa mbalimbali zilizowasilishwa katika kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya 


Habari kamili.....                                                                                      


Kiteto yafanya kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya


Wilaya ya kiteto imefanya kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya  baada ya miaka mitano.Mara ya mwisho kikao hicho kilifanyika mwaka 2013.Akimkaribisha mwenyekiti  kwa ajili ya kufungua kikao hicho, katibu tawala wa wilaya ya Kiteto ndugu Stephano  Ndaki amesema  kwamba vikao hivyo vimekuwa havifanyiki kwa muda mrefu kutokana  na gharama za kuviendesha kuwa kubwa kwa sababu  ilikuwa ni lazima wajumbe walipwe posho, jambo ambalo lilikuwa linasababisha vikao hivi kutokukaa, lakini kwa utaratibu wa sasa  vikao hivyo vitakaa  kwa gharama nafuu, ambayo ni gharama ya chakula na nauli  kwa wajumbe  wanaotoka  mbali sana, kwani  umuhimu wa vikao hivyo ni mkubwa  sana kuliko kuangalia zaidi kupata posho halafu wakashindwa kukaa.

Akifungua kikao hicho mkuu wa wilaya ya Kiteto  mheshimiwa Tumaini magesa ambaye kwa mujibu wa sheria ndiye mwenyekiti, amesema  kwamba  migogoro ya wakulima na wafugaji imeendelea kutatuliwa , na  wao  kama viongozi  kazi yao ni kuhakikisha kuwa migogoro hiyo inakwisha , japokuwa kawaida ya Kiteto inaeleweka kwamba  kila  wanapotatua mgogoro mmoja ,yule ambaye  katika utatuzi wa mgogoro anaona  haki haikuwa  kwa upande wake ,   anadhani mwenzake ametoa rushwa. Lakini anaamini kwamba  watakuwa  wanakwenda vizuri kadiri  watatakavyokuwa  wanakutana katika vikao kama hivyo kwani mambo yote ili yaweze kwenda vizuri  ni muhimu  kuwa wanakutana kwenye vikao, watakapokuwa wanakutana  migogoro itakuwa inakwenda ikipungua kwa sababu kila mmoja atakuwa anajua kinachoendelea.

Kwa  upande wa  ulinzi na usalama, mwenyekikiti   amesema kwamba  hali ya ulinzi na usalama  katika wilaya ya Kiteto imeimarika ,kuna matukio machache ya  uhalifu, lakini  vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi yake, na  kuwataka wajumbe  tuviruhusu vyombo hivyo vifanye kazi . Aidha mwenyekiti  amewahakikishia  wajumbe wa kikao hicho kwamba   yeye  kwa  kushirikiana  na kamati yake ya ulinzi na usalama  ya  wilaya wanaendelea kupambana  kuhakikisha  kwamba  wanafika mahali ambapo  wilaya ya Kiteto  itakuwa imetulia ,na kwamba ikitulia  kila mmoja atafanya shughuli za maendeleo katika utaratibu ambao unakubalika na serikali na atakula matunda ya uhuru.
Katika kikao hicho taarifa mbalimbali ziliwasilishwa, wajumbe walizijadili na kutoa ushauri ambapo katika taarifa ya bajeti ya mwaka 2017/18 wajumbe walishauri kwamba  ni vyema halmashauri  ikajikita  zaidi  katika ukusanyaji wa mapato kwa kuwa fedha zinazoletwa na serikali kuu  hazilingani na kazi na miradi ambayo halmashauri inapaswa kuitekeleza, hali ambayo inasababisha kukwama kwa miradi ya maendeleo. Wajumbe walishauri  kwamba minada iliyokuwepo miaka ya 1980  ya Kijungu na Ndedo  ifunguliwe  na maeneo mengine mazuri yatafutwe ili  kuwezesha biashara ya mifugo  kuiletea halmashauri  ya wilaya ya Kiteto mapato na siyo  wilaya  jirani  kama ilivyo sasa. Wajumbe walishauri kwamba  halmashauri iweke utaratibu wa kutoa elimu  kwa wakulima na wafugaji  wakubwa ili kuanza  kuchangia maendeleo kwa mwaka.
Vilevile wajumbe walishauri  mamlaka ya mji mdogo wa Kibaya iendelee kutafuta  vyanzo vya mapato ili kuiwezesha kujiendesha vizuri.Aidha wajumbe walishauri elimu iendelee kutolewa  kwa kata za Njoro na Partimbo  ili waridhie kuwa sehemu  ya mamlaka ya mji mdogo wa Kibaya.Wajumbe walishauri kwamba ili kupata mapato ni vyema mabaraza ya kata ambayo yalivunjwa  kwa mujibu wa sheria yaundwe kabla ya mwezi Desemba 2017, kwani mabaraza hayo ni moja wapo  ya  vyanzo  vya mapato vya halmashauri. Kwa upande wa ukusanyaji mapato  wa TRA   wajumbe walishauri kwamba elimu zaidi itolewe  kwa wafanyabiashara juu ya matumizi ya mashine za kutolea risiti za kielekroniki  yaani EFD.Na watumiaji wa huduma  mbalimbali waelimishwe juu ya umuhimu wa kudai risiti.
Katika kujadili suala la migogoro ya ardhi,wajumbe walishauri kuwa wataalamu pamoja na viongozi wasimamie matumizi bora ya ardhi ili kuondoa migogoro.Aidha walishauri kuwa miundo mbinu katika maeneo ya kilimo na ufugaji  iboreshwe ili kuwezesha wahusika kufanya shughuli zao bila migogoro na kwa usalama zaidi,katika kipengele cha  usalama wa watu na mali   zao, wajumbe walisisitiza zaidi juu ya alama za barabarani kwa ajili ya kuonyesha maeneo ya kuvukia binadamu na mifugo,hususani katika barabara kuu.

Katika suala la afya,wajumbe walishauri elimu na hamasa itolewe zaidi kwa jamii ili jamii iweze kuona umuhimu wa kujiunga na bima ya afya  iliyoboresha ,ili kupunguza gharama za matibabu ,na kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wote ili waweze kufanya shughuli za kiuchumi na kujiletea maendeleo.Aidha baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya hali ya vyoo  katika wilaya, wajumbe walishauri halmashauri kuweka  mkakati maalum wa kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa vyoo na matumizi ya vyoo ,halmashauri iweke faini kwa kaya ambazo zitakuwa hazikujenga vyoo katika muda  fulani ambao utakuwa umepangwa ili kudhibiti hali ya uchafu katika mazingira ya wilaya na kuzuia milipuko ya magonjwa.Wakati huohuo  wajumbe walipokea taarifa ya maandalizi ya kilimo kwa mwaka 2017/2018 na walishauri kuwa elimu ya hali ya hewa iwafikie  wananchi wote ili kujiandaa kwa kilimo kulingana na hali ya hewa .Pia wajumbe walishauri juu ya suala la ruzuku  ya pembejeo kufuatiliwa  mapema na idara husika ili kujua kama zinapatikana.

Katika hatua nyingine wajumbe waliweka maazimio ishirini (20),ambapo maazimio hayo yaliafikiwa baada ya mijadala ya kina iliyotokana na taarifa  zilizowasilishwa na wataalamu mbalimbali wa halmashjauri na mamlaka ya mapato  wilaya ya Kiteto. Maazimio hayo ni kuboresha mapato ya halmashauri ya wilaya kwa kuongeza vyanzo vya mapato na kuwa na vitega uchumi.Wadau kuendelea kushirikiana na TRA  ili kuhakikisha kwamba mapato ya serikali yanakusanywa ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Taarifa ya  kutowasilishwa kwa fedha za miradi ya maendeleo iwasilishwe kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC)  ili  kamati hiyo iweze  kusaidia kusukuma jambo hilo, ili fedha hizo ziweze  kuwasilishwa kwa wakati. Viongozi wa wilaya wafuatilie moja kwa moja katika wizara husika fedha  za miradi  ya maendeleo. Minada iboreshwe  kwa kujenga miundo mbinu kama vile vyoo,barabara , sehemu za kuingilia na kutokea mifugo, kuweka uzio ili kuzuia watu kutorosha mifugo kabla ya kuilipia ushuru. Halmashauri ianzishe minada katika maeneo ya Ndedo na Kijungu. Mabaraza ya kata yawezeshwe kwa kupatiwa  mafunzo na vitendea kazi.Elimu itolewe kwa wafugaji, wapeleke mifugo minadani na  badala ya  kuuzia  majumbani. Alama za barabarani ziwekwe  ili kutambua vivuko vya binadamu na mifugo.Wadau waendelee kuhamasishwa kuingia katika uchumi wa viwanda. Vijiji vitoe maeneo ili kuvutia wawekezaji,aidha  halmashauri ya wilaya pamoja na vijiji viendelee kutenga maeneo hayo.Vijiji vizingatie matumizi bora ya  ardhi. Mabwana afya wasimamie usafi ipasavyo badala ya kukaa ofisini. Katika zile siku maalumu zilizoamriwa za kufanya usafi, wananchi wote washiriki katika usafi wa mazingira,biashara zote zifungwe. Kuwepo na tathmini ya elimu katika ngazi ya vijiji hadi katika  ngazi ya halmashauri ya wilaya . Vijiji ambavyo havina shule ,ifikapo  2018 viwe na shule mfano Ngapapa.Kuboresha miundo mbinu ya shule  mfano madarasa, vyoo na nyumba za walimu .Wananchi  waelimishwe namna ya uchangiaji  wa mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa. Serikali  ishauriwe juu ya fedha za TASAF,  fedha za TASAF III zielekezwe zaidi kwenye miradi ya maendeleo ambapo itanufaisha watu wengi zaidi kuliko inavyofanyika sasa ambapo kaya maskini hupewa fedha hizo lakini wengi wao wanaopewa fedha hizo huzitumia vibaya mfano kuongeza wake, kulewa , matumizi ambayo  husababisha fedha hizo kutokuwanufaisha hata wao wenyewe.Wakulima  na wafugaji wahamasishwe  kulima na kufuga kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo na ufugaji bora ili mifugo na kilimo hicho viweze kuwaletea maendeleo na pia kutoharibu mazingira .

Akifunga kikao hicho mwenyekiti aliwashukuru wajumbe wote kwa kushiriki katika kikao hicho na kusisitiza kuwa maazimio yaliyofikiwa yafanyiwe kazi kwa wakati .Aidha kikao kingine cha kamati hiyo kitafanyika mnamo mwezi wa tatu mwaka 2018.

Kikao cha kamati ya ushauri  ya wilaya  ni kikao cha juu katika wilaya. Kikao hiki  hukaa mara mbili kwa mwaka, mwezi wa tatu na mwezi wa kumi.  kikao hiki hukutana  kupokea na kupitia mpango wa maendeleo wa halmashauri na kisha kushauri ili utekelezaji uweze kufanyika  ipasavyo, kupitia taarifa mbalimbali za miradi mbalimbali ya kitaifa na kuweza kushauri, kusimamia na kushauri uendeshwaji wa taasisi zisizokuwa za kiserikali kwenye wilaya na kusimamia na kuhakikisha kwamba halmashauri inatekeleza mpango wake wa bajeti kama ilivyokusudiwa . Kamati ya ushauri ya wilaya  iliundwa kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 2006 kipengele cha 15a – 15 b  ambapo mwenyekiti wa kikao cha kamati hiyo ni mkuu wa wilaya.


Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa