Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto imepata hati safi katika mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023.
Kauli hiyo imetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa, Bw. Abdalla Shaib Kaim, Oktoba 8, 2023 Wilayani Simanjiro wakati Kiteto ikikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Wilaya ya Simanjiro.
Bw. Kaim alisema, Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Manyara ulipokelewa katika Wilaya ya Kiteto na wilaya hiyo imefanya vizuri na kupata hati safi. ‘Huo ni mwanzo mzuri kwa Mkoa wa Manyara ninaamini Simanjiro na wilaya nyingine za mkoa huu nazo zitafanya vizuri”, aliongeza Bw. Kaim.
Bwana Kaim pia alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, SSI. Mbaraka Alhaj Batenga, Mkurugenzi Mtendaji (W), CPA. Hawa Abdul Hassan , wataalamu wote na wananchi kwa utekelezaji na usimamizi mzuri wa miradi hiyo mizuri.
Sambamba na hilo, nae Mkimbiza Mwenge wa Taifa, Bi. Atupokile Elia Mhalila, aliipongeza Kiteto kwa kua na mradi bora wa afya. “Toka tulipoanza kukimbiza Mwenge wa Uhuru 2023, hatujakutana na mradi mkubwa wa afya na uliotekelezwa kwa ubora wa kiwango kile kupitia force akaunti”, aliongeza Bi Mhalila.
Oktoba 7,2023 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Queen Cuthbert Sendiga aliupokea Mwenge wa Uhuru kimkoa katika viwanja vya shule ya msingi Dosidosi Wilayani Kiteto na kisha kuukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya Mh Batenga. Ukiwa wilayani Kiteto, Mwenge wa Uhuru umekimbizwa umbali wa takribani kilometa 208 na umepitia miradi 9 ambapo miradi 3 ilifunguliwa, miradi 2 ilizunduliwa, mradi 1 uliwekewa jiwe la msingi na miradi 3 kukaguliwa; yote ikiwa na jumla ya thamani ya bilioni 2.4. Miradi hiyo ni pamoja na miradi ya sekta ya elimu, afya, maji na utunzaji wa mazingira.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa