Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ,watumishi wa taasisi mbalimbali za serikali, watumishi wa taasisi binafsi pamoja na wakazi wa mji mdogo wa Kibaya wilayani Kiteto wameungana na watanzania wengine kufanya usafi katika kuazimisha siku ya usafi kitaifa ambapo watumishi wamefanya usafi katika sehemu zao za kazi, na wakazi wa mji mdogo wa Kibaya wamefanya usafi katika mazingira yanayozunguka makazi yao.
Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku ya usafi kitaifa. Ambapo kwa mwisho wa mwezi Februari 2018 ilikuwa ni Jumamosi ya tarehe 24 .
Wakuu wa idara mbalimbali za halmashauri pamoja na Meneja wa TARURA wilaya ya Kiteto wakifanya usafi katika mazingira yanayozunguka ofisi za halmashauri (Bomani) zilizopo katika mji mdogo wa Kibaya
Watumishi kutoka idara mbalimbali za halmashauri pamoja na TARURA wilaya ya Kiteto wakifanya usafi katika mazingira yanayozunguka ofisi za halmashauri (Bomani) zilizopo katika mji mdogo wa Kibaya .
Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ( idara ya afya tiba )wakifanya usafi katika maeneo mbalimbali ndani ya hospitali ya wilaya ya Kiteto iliyopo katika mji mdogo wa Kibaya .
Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Kiteto wakifanya usafi katika mazingira yanayoizunguka mahakama hiyo iliyopo katika mji mdogo wa Kibaya .
Watumishi wa Benki ya NMB tawi la Kibaya wakifanya usafi katika mazingira ya benki hiyo iliyopo katika mji mdogo wa Kibaya wilayani Kiteto.
Waumini wa dini ya Kiislamu wakifanya usafi katika mazingira ya nyumba yao ya ibada (Msikiti) iliyopo katika mji mdogo wa kibaya wilayani Kiteto.
Wakazi wa mji mdogo wa Kibaya wilayani Kiteto wakifanya usafi katika mazingira ya makazi yao .
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa