Mh.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo Akizungumza na Wananchi Katika Uzinduzi wa Kituo Cha Afya cha Kata ya Sunya Katika Halmashauri ya Wilaya Kiteto Mkoa wa Manyara Tarehe 14.05.2020.
Mh.Waziri Jafo (watatu kutoka kulia) Akikagua na Kuzungumza na Viongozi Katika Chumba cha Upasuaji Ambapo Kitanda Maalumu cha Wagonjwa Kimefungwa Kama Inavyoonekana Kwene Picha ya Hapo Juu.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim Kambona Akiwasilisha Taarifa ya Ujenzi wa Kituo Husika kwa Mh. Waziri Jafo.
Mh. Waziri Jafo Akizindua Kituo Hicho.
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhandisi,Tumaini Magessa Akizungumza Katika Uzinduzi Huo.
Mh. Mbunge wa Wilaya ya Kiteto Emmanuel Papian Akizungumza Katika Uzinduzi Huo.
Muonekano wa Juu wa Kituo cha Afya cha Sunya Wilayani Kiteto Mkoani ManyaraMh.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo Akizungumza na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Katika Ukaguzi wa Jengo la Halmashauri.Jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mei 14, 2020
-------------------------------------------------- HABARI KAMILI --------------------------------------------------
Haya yote yamejiri tarehe 14.05.2020 na Mh.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo alipokuwa akizindua kituo hicho kilichopo Kata ya Sunya umbali wa kilometa zaidi ya 100 kutoka makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto baada ya kukagua na kurishwa na ubora wake ukilinganisha na gharama zilozotumika. Mh. Waziri Jafo amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda miundombinu yote ya kituo kwani ni mradi wao na wanaonufaika na huduma za afya ni waona maeneo mengine ya jirani.
Katika uzinduzi huo Mh. Jafo amesema kituo hicho ndani ya wilaya hiyo ni msaada mkubwa sana kwa wananchi wa hapo na kitakuwa kimetatua changamoto nyingi ikiwemo kukosekana kwa kituo cha afya katika kata ya Sunya hali iliyowalazimu awali wakazi hao kusafiri umbali mrefu kupata huduma kama hii, tunamshukuru Mh. Rais Dkt J.P.Magufuli kwa kutoa fedha shilingi milioni 400 ili kujenga kituo hiki katika Wilaya ya Kiteto kwa lengo kuu la kuboresha huduma za afya kwa wananchi katika nchi yetu na ninaupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkurugenzi Mtendaji Bw. Tamim Kambona na Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhandisi Tumaini Magessa kwa usimamizi mzuri unaoendana na kasi ya awamu ya serikali ya tano.Katika uinduzi huo Mh.Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhandisi,Tumaini Magessa ameiomba serikali kuwaongezea vituo vya afya viwili ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kutokana na ukubwa wa Wilaya ambayo ina kilometa za mraba 16,865. Mh. Mkuu wa Wilaya Mhandisi Tumaini Magessa amebainisha changamoto kubwa iliyopo kwa sasa katika kituo hicho ni ukosefu wa umeme wa gridi ya Taifa, hivyo kulazimika kutumia jenereta ambapo gharama za uendeshaji ni kubwa. Aliongeza kwa kusema “Mh. Waziri wa Nishati alikuja wiki kadhaa zimepita ameridhia kuleta umeme hadi hapa Sunya katika kituo hiki”
Akitoa taarifa ya ujenzi huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamimu Kambona amesema ujenzi huo ulianza januari 2018 na umekamilika mwaka 2019 kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 510 na wananchi elfu 38,273 wanatarajiwa kunufaika na huduma ya afya katika kituo hiki. Hata hivyo kiasi cha shilingi milioni 483.4 zimekwishatumika huku milioni 35.0 zimebaki ambazo zitatumika kujenga duka la dawa. Ni wazi kwamba uwepo wa kituo hiki kutasaidia kuondoa adha ya kutembea umbali mrefu waliyokuwa wanapata wananchi katika kupata huduma za afya pia kutapunguza vifo vya mama wajawazito na watoto,”
Akizungumza katika uzinduzi huo Mh. Mbunge wa Wilaya ya Kiteto Emmanuel Papian kwa niaba ya wananchi ameishukuru serikali kwa kukamilisha kituo hicho na kumuomba waziri afikishe salamu zao kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli. Awali kabla hajafika katika kituo cha Afya cha cha Sunya, Mhe. Jafo alikagua ujenzi wa jengo la Halmashauri na kumtaka mkandarasi wa Pacha Construction LTD kukamilisha ujenzi kwa wakati.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa