Katika mipango na mikakati ya serikali ya kuboresha na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi, kituo cha afya cha Engusero kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kimeanza kufanya upasuaji kwa mama wajazito.
Akizungumza kuhusu huduma hiyo Oktoba 12, 2023, Mganga Mkuu (W), Dr. Vicent Gyunda amesema kwamba upasuaji wa kwanza umefanyika Oktoba 3, 2023 ikiwa ni baada ya kituo hicho kupokea vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 105,000,000 kutoka serikali kuu.
“Ni shukrani za kipee kwa Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwasogezea karibu huduma za afya wananchi wa Kiteto” alisema Dr. Gyunda.
Nae Mkurugenzi Mtendaji (W), CPA. Hawa Abdul Hassan, amesema kwamba katika mwaka wa fedha 2022/2023 halmashauri yake ilipokea kiasi cha takribani bilioni 1.5 katika sekta ya afya ambapo kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi 900,000,000 zilitumika kujenga majengo matatu katika hospitali ya wilaya, ambayo ni jengo la mama na mtoto, jengo la maabara na jengo la upasuaji.
Vilevile halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi 100,000,000 kwaajili ya ukamilishaji wa maboma ya zahanati. Sambamba na hilo, halmashauri ilipokea pia kiasi cha shilingi 100,000,000 kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya zahanati ya Njiapanda, Magungu, Nchinila na Ngipa.
Upande wa ununuzi wa vifaa tiba katika vituo vya afya Engusero, Mwanya na Kijungu;, halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi 450,000,000 na vifaa tiba vyote upande wa zahanati na vituo vya afya vimekwisha nunuliwa.
“Katika mwaka huu wa fedha 2023/2024, mpaka sasa halmashauri imekwisha pokea kiasi cha shilingi 936,000,000 ambapo kati ya hizo sekta ya afya imepokea kiasi cha shilingi 100,000,000 kwaajili ya ukamilishaji wa maboma ya zahanati mbili ambazo ni zahanati ya Mbeli iliyopo kijiji cha Kimana kata ya Partimbo na zahanati ya Olgira iliyopo kijiji cha Olgira kata ya Sunya”, alisema Mkurugenzi Mtendaji, CPA. Hawa Abdul Hassan.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa