Madaktari wa Kituo Cha Afya cha Sunya Wakiwa Katika Chumba Maalumu cha Upasuaji Wakifanya Upasuaji wa Mama Mjamzito
------------------HABARI ------------------
Ndani ya wiki chache baada ya Mh.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo kuzindua kituo hiki sasa kituo kinafanya upasuaji mdogo hadi mkubwa hii ni ishara njema sana kwa wananchi kuwa changamoto ya kuhangaika kwa wananchi hususani kundi la akina mama wajawazito sasa lapata mwarobaini.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto Dkt Paschal Mbota ambaye ndiye aliyeratibu shuguli hii amesema "huu ni upasuaji mkubwa wa kwanza, kwa hiyo hakuna rufaa ya mama mjamzito tena"
Shukrani za pekee kwa Mh.Rais, Dkt J.P.Magufuli kwa kutoa fedha milioni 400 na vifaa mbalimbali vya kituo hiki pamoja na vifaa vya upasuaji, ufuatiliaji mzuri wa Mh.Waziri Jafo, Uongozi wa Wilaya ya Kiteto na wataalamu wa afya Hospitali ya Wilaya na Kituo husika wanaohusika katika kazi hii.
Malengo ya Serikali ya awamu ya tano yametimia hivyo wananchi sasa ni kuendelea kuiamini serikali yao na kukitunza kituo hiki ili kiendelee kutoa huduma bora daima kwa wananchi.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa