Shirika la Standing Voice kwa kushirikiana na Kitengo cha Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, Aprili 21, 2025, limeendesha huduma ya kliniki ya ngozi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi wilayani Kiteto.
Katika kliniki hiyo jumla ya watu 25 kutoka katika kata ya Kibaya, Njoro, Kaloleni na Bwagamoyo walifika katika Hospitali ya Wilaya kupata huduma hiyo. Aidha huduma hiyo huyolewa katika vituo vya Afya Engusero na Sunya.
Katika kliniki hiyo kila mmoja ameweza kupatiwa chupa (tube) 3 za mafuta maalumu kwaajili ya kutunza ngozi zao na kofia moja moja.
Aidha wamepatiwa elimu ya kujikinga na jua, ikiwa ni pamoja na uelimishaji kwa njia ya vipeperushi.
Mkuu wa Kitengo cha Ustawi wa Jamii, Ndg. Jackline Barongo, amesema kwamba wilaya ya Kiteto ina jumla ya walemavu wa ngozi 43, hivyo Halmashauri kupitia Kitengo hicho, inaendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa huduma hii ili kuweza kuwahudumia walemavu wa ngozi wote kwani wengine hushindwa kujitokeza kwa kukosa uelewa juu ya umuhimu wa huduma hiyo.
Huduma hiyo ambayo imeanza kutolewa wilayani Kiteto tangu mwaka 2021, hufanyika kila baaada ya miezi mitatu.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa