Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ilifanya kongamano la uzinduzi wa msimu wa kilimo 2024/2025 tarehe 20 Desemba 2024. Lengo lilikuwa kuhamasisha wakulima, wadau wa kilimo, na watoa huduma za ugani kujadili fursa na changamoto za kilimo.
Kiteto, ambapo zaidi ya asilimia 90 ya wakazi wanategemea kilimo, bado inakabiliwa na changamoto za tija ndogo ya uzalishaji. Katika msimu wa 2023/2024, ekari laki tatu za mahindi zililimwa, lakini tija ilikuwa tani 0.5-0.6 kwa ekari, kutokana na upatikanaji duni wa pembejeo bora na elimu ya kilimo.
Serikali imeanzisha mpango wa ruzuku ya mbegu na mbolea kwa lengo la kuongeza uzalishaji na kupunguza gharama kwa wakulima. Hata hivyo, wakulima 18,901 tu wamejisajili kati ya zaidi ya 100,000 waliopo wilayani, hivyo kuhimiza usajili zaidi.
Wilaya inalenga kulima hekta 284,270 na kuzalisha tani 485,409 za mazao kwa mwaka 2024/2025. Kaulimbiu ya kongamano ilikuwa “Tuongeze tija na uzalishaji kwa matumizi sahihi ya mbinu na teknolojia bora za kilimo na mifugo.”
Kongamano lilijumuisha mafunzo ya afya ya udongo, matumizi ya pembejeo bora, na usajili wa wakulima kwenye mfumo wa ruzuku. Wakulima walihimizwa kushiriki kikamilifu ili kunufaika na mpango huu wa maendeleo ya kilimo.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa