Viongozi wa dini Wilayani Kiteto wameombwa kwenda kuwapa elimu waumini wao juu ya madhara ya rushwa katika uchaguzi wa serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba, 2024.
Rai hiyo imetolewa Septemba 28, 2024 na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara, Ndg. Bahati Stafu Haule, katika semina maalumu na Masheikhe, Maimamu na Makatibu kata wa misikiti Wilayani Kiteto.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Kiteto, Ndg, Venance Sangawe, amesema kwamba lengo la semina hiyo ni kupanua wigo na ushirikiano na wadau haswa katika kipindi hiki cha uchaguzi ili kuwezesha jamii kuwa macho juu ya vitendo vya rushwa katika mchakato wote wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Akitoa semina hiyo, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara Ndugu Bahati Stafu Haule amesema kwamba viongozi wa dini hao wana nafasi kubwa ya kukemea rushwa maana rushwa ni suala mbali ya kuwa ni Jinai la pia kiimani kwani vitabu vyote viwili vya dini, Quran Tukufu na Biblia Takatifu, vinakataza vitendo vya rushwa na kwamba ni dhambi.
Mkuu huyo ameeleza kwamba katika uchaguzi, rushwa inaweza kutokea katika mazingira matatu ambayo ni kwa mgombea, kwa mpiga kura na kwa msimamizi wa uchaguzi hivyo wananchi wanatakiwa kuhakikisha kuwa vitendo vya rushwa havitokei hasa kabla, wakati na baada ya Uchaguzi.
“Kiongozi anayekupa rushwa ili umchague ina maana hafai kuwa kiongozi ndio maana anatumia nguvu ya ziada achaguliwe. Kiongozi anayepatikana kwa njia ya rushwa akiwa madarakani hawezi kuleta maendeleo kwani atakua anafanya kazi kwa maslahi yake binafsi ili aweze kurudisha gharama alizozitumia kwenye uchaguzi”, ameongeza Ndg. Haule.
Mkuu huyo aliendelea kufafanua kuwa TAKUKURU ina majukumu makuu mawili ambayo ni Kuzuia na Kupambana Rushwa ambapo majukumu ambapo jukumu la Kuzuia linatekelezwa kupitia utoaji elimu, tafiti, chambuzi za mifumo na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo aidha katika kupambana alielezea kuwa jukumu hilo linatekelezwakupitia hayo wanayatekeleza kupitia Uchunguzi na Mashtaka.
Mkuu huyo ameongeza kwa kusema kwamba TAKUKURU peke yao hawawezi kutomeza rushwa bali ushirikiano kati yao na taasisi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini na hiyo ndio sababu ya semina hiyo ili kupeana elimu kwa lengo la viongozi hao kwenda kuelimisha waumini wao.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto, Bi. Mufandii Msaghaa , amewashukuru viongozi wa TAKUKURU Wilaya na Mkoa kwa kuona umuhimu wa kutoa elimu hiyo kwa viongozi hao wa dini na kusema kwamba elimu hiyo imekuja wakati muafaka kwani taifa linajiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika Novemba 27,2024.
Naye Sheikhe wa Wilaya ya Kiteto, Sheikhe Omari Bakari Fumito, ameishukuru taasisi hiyo ngazi ya Wilaya na Mkoa, kwa elimu waliyowapatiwa na kuwahimiza masheikhe hao na maimamu kuwa elimu hiyo iwanufaishe na kuwafikia waumini wanaowaongoza.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa