Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga leo Julai 19,2025, amemkabidhi Mwenge Wa Uhuru 2025 Mkuu wa mkoa Wa Singida Mhe. Halima Omary Dendego.
Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru 2025 yamefanyika Katika kijiji cha Sagara kata Itaja Halmashauri ya Wilaya ya Singida.
Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika Halmashauri Saba (07) ambazo ni Kiteto,Simanjiro, Hanang,Halmashauri ya Mji wa Mbulu na Babati, Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Mbulu Mkoani wa Manyara kuanzia tarehe 12 -18 Julai,2025.
Mwenge wa Uhuru 2025 Umeridhia Miradi 53 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 71.3 kwa 100% Mkoani Manyara.
Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 inasema “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”
KWAHERI MWENGE WA UHURU 2025 MKOANI MANYARA.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa