Mh.Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Kanali Patrick Songea (aliyesimama) Akifungua Kikao cha Kamati ya Lishe ya Wilaya Kilichofanyika Tarehe 26.08.2020 Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.kulia kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto Bi. Neema Nyalege na kushoto kwake niMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim Kambona
Wajumbe mbalimbali wa Kamati ya Lishe Wakiwa kwene Kikao Hicho Kama Wanavyoonekana Kwene Picha Hapo Juu
--------------------------- HABARI KAMILI ---------------------------
Haya yamejiri katika kikao cha Kamati ya Lishe ya Wilaya ya Kiteto kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri tarehe 26.08.2020, imefahamika kwamba wanajamii wengi wasiopata lishe bora hupatwa na magonjwa ya utapia mlo (udumavu).
Hasa kwa watoto na watu wazima ni sukari, shinikizo la damu, kansa na mengineyo. Kitaalamu inashauriwa mbali na kuwa na lishe bora inatakiwa kila mwanajamii kuwa na tabia ya kupima afya mara kwa mara hali inayopelekea kufahamu afya yako na kujiwekea kinga kabla ya hali yaugonjwa kuwa mbaya, “kinga ni bora kuliko tiba”.
Katika utekelezaji wa shuguli za lishe ndani ya wilaya zinashirikishwa idara/vitengo mtambuka na taasisi mbalimbali zikiwemo za kidini ili kuwepo kwa uelewa mpana kwa jamii. Baadhi ya idara/vitengo hivyo ni Elimu Msingi, Elimu sekondari, Mipango, Afya, Kilimo, Mifugo, Fedha, Tehama, Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii, Wakala wa Maji Mijini na Vijiji (RUWASA), Huku taasisi zingine za kidini ni Bakwata na za Kikristo na Jumuiya za wenye viwanda vya usindikaji vyakula na mafuta kiteto.
Mwisho Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe Mh.Mkuu wa Wilaya Kanali Songea, amesema “changamoto zilizopo ndani ya wilaya zifanyiwe kazi na kila mmoja ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Lishe anapaswa aonekane katika kuinua kiteto”
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa