• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wilaya ya Kiteto yatekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya kukuza uchumi wa viwanda

Imetumwa : September 15th, 2017

                                                                                                                                    

                 Kiongozi wa mbio za mwenge ndugu Amour Hamad Amour akisikiliza maelekezo ya jinsi mashine zinavyofanya kazi katika kiwanda cha Kwadelo Sunflower and Super kabla ya uzinduzi wa kiwanda hicho kilichopo katika kata ya Matui.Aliyesimama kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Kiteto Mh. Tumaini Magessa

                                                                                                                                                                

                                                                                                                                                                 

               Jengo la wodi ya wanawake na watoto lililozinduliwa na   Mwenge  wa uhuru katika kata ya Matui .

Jengo la madarasa yaliyozinduliwa na mwenge katika shule ya sekondari Engusero.


           Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Amour Hamad Amour akikagua darasa lililozinduliwa na mwenge katika shule ya sekondari Engusero katika kata ya Engusero.Walioambatana nae ni mkuu wa wilaya ya Kiteto Mh. Tumaini Magessa,mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kiteto Ndg. Tamim Kambona na maafisa wengine wa serikali wilayani Kiteto.



Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Amour Hamad Amour akifungua mradi wa maji katika kata ya Kaloleni.


HABARI KAMILI

Wilaya ya Kiteto yatekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya kukuza uchumi wa viwanda.

Wilaya ya Kiteto imetekeleza kwa vitendo kauli mbiu  ya mwenge wa uhuru mwaka  2017 ambayo ni shiriki  katika kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu, kwa kuanzisha  kiwanda cha kukamua alizeti na kusaga mahindi.Kiwanda hicho kilichopo katika kata ya  Matui  ni miongoni mwa miradi minne iliyozinduliwa na mwenge wa uhuru wilayani kiteto.Mradi  huo wa kiwanda una thamani ya shilingi 400,050,000.

Miradi mingine iliyozinduliwa na mwenge wa uhuru  ni madarasa  mawili  yaliyojengwa katika shule ya sekondari  Engusero iliyopo  katika kata ya Engusero .Mradi huo wa madarasa una thamani ya shilingi 26,740,120,ambapo halmashauri imechangia shilingi 865,000  . Pia Kikundi cha vijana Kaloleni kilizinduliwa ,kikundi hicho kilianzishwa kwa lengo la kuwawezesha vijana kuendesha shughuli za kiuchumi na kukuza kipato cha kila kijana kwenye kikundi , kina miradi mbali mbali kama ufugaji kuku  chotara, uuzaji wa vifaranga na mayai, kilimo cha mbogamboga, biashara ya bodaboda na VIKOBA, miradi yote hiyo ya kikundi cha vijana  ina thamani ya shilingi 8,200,000 ,ambapo  halmashauri  ya wilaya  ilikipatia kikundi hicho mkopo wa shilingi  2,000,000,fedha  ambayo  ilitumika  kununua  pikipiki, ambayo inawawezesha vijana  hao kupata marejesho  na kuendesha shughuli nyingine za kikundi. Mradi mwingine uliozinduliwa ni kampeni  ya kutokomeza  malaria, wilaya ya Kiteto ilianzisha kikundi  cha kupambana na kutokomeza  ugonjwa  wa malaria.Mradi huo una thamani ya shilingi 500,000,ambapo fedha hizo zilitolewa na halmashauri .

 

 Kadhalika  mradi wa ujenzi wa jengo la wodi ya wanawake  na watoto  umewekewa jiwe la msingi.Mradi huo  wa wodi upo katika kata  ya matui na una thamani ya shilingi 37,796,000,  halmashauri ya wilaya ya Kiteto imechangia shilingi 20,246,000 .

Sambamba na hayo, mradi wa maji ulifunguliwa . Mradi huo uko katika kata ya Kaloleni na  una thamani ya shilingi 255,915,500, kati ya fedha hizo ,halmashauri imechangia shilingi  5,000,000.

Katika  hatua  nyingine  miradi miwili ilikaguliwa. Miradi hiyo ni Kikundi cha wanawake, kikundi hicho kilianzishwa kwa lengo la kuwawezesha wanawake  kuendesha shughuli za kiuchumi na kukuza kipato na kina miradi kama kufuma mashuka ya kimasai ushanga ,kutengeneza shanga,hereni na mikufu ,usindikaji vyakula , uuzaji wa bidhaa mbalimbali kama sukari ,mchele na sabuni  na VICOBA. Miradi yote  hiyo ya kikundi cha wanawake ina  thamani ya shilingi 10,500,000. Mradi mwingine uliokaguliwa ni mradi wa utunzaji wa mazingira, ambapo  zoezi la upandaji miti  katika eneo la shule ya Sekondari  Engusero lenye ukubwa wa ekari 2.5 lilifanyika ikiwa ni sehemu ya utunzaji mazingira katika wilaya ya Kiteto. Mradi huo una thamani ya shilingi 1,420,000, ambapo halmashauri imechangia shilingi 160,000.

Mwenge wa uhuru umepokelewa wilayani Kiteto na mkuu wa wilaya ya Kiteto mheshimiwa Tumaini Magesa,  ambapo umepitia katika tarafa  tatu,kata saba ,vijiji kumi na tano  na kukimbizwa umbali wa kilometa 90 kutoka eneo la mapokezi hadi eneo la mkesha.Jumla ya miradi 8 imepitiwa na mwenge wa uhuru , thamani  ya  miradi yote  iliyopitiwa ni shilingi za kitanzania 750,571,120, ambapo wadau wa maendeleo wamechangia shilingi 17,210,000 , Jamii shilingi 444,900,00, halmashauri ya  wilaya ya Kiteto shilingi 28,771,000 na serikali kuu shilingi 259,690,120.






Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPTEMBA 2023 September 03, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABIA MBAYA ZA WATUMUSHI ZINAHARIBU SIFA ZA TAASISI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LIMEMPONGEZA RAIS SAMIA.

    May 30, 2025
  • PONGEZI KWA WANANCHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

    April 28, 2025
  • TUUENZI MUUNGANO WETU

    April 27, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa