Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Fakii Lulandala, Aprili 15, 2025, ameongoza kikao cha Kamati ya Maandalizi ya kuupokea Mwenge wa Uhuru 2025 unaotarajiwa kupokelewa na kukimbizwa wilayani hapo Julai 13,2025.
Kikao hicho kilichohudhuliwa na wadau mbalimbali kutoka serikalini na sekta binafsi, kilikua na lengo la kuanza kuanisha miradi itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2025 na kuunda kamati ndogondogo kwaajili ya maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2025.
Mwenyekiti wa Kikao hicho, Mhe. Lulandala, aliwasihi wanakamati hao kufanya maandalizi mapema kwani muda sio rafiki. Maandalizi hayo ni pamoja kuwafikishia wananchi taarifa ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 ili nao waweze kujiandaa kuipokea tunu hiyo ya Taifa.
Aidha, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto, Ndg. Mufandii Msaghaa, aliwasihi wataalamu wote wanaohusika kwenye miradi kuhakikisha wanasimamia vizuri miradi hiyo na kuhakikisha nyaraka zote muhimu zinaandaliwa vizuri.
Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge mwaka 2025 ni “ Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa