Mgeni Rasmi katika maazimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Mbigiri - kata ya Partimbo wilayani Kiteto ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe.Tumaini Magessa (aliyesimama) akihutubia wananchi wakati wa maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbigiri akiwasalimia wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Mbigiri - kata ya Partimbo wilayani Kiteto.
Katibu wa UWT (W) Kiteto Bi. Fatuma akiwasalimia wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Mbigiri - kata ya Partimbo, wilayani Kiteto.
Kaimu Katibu Tawala (W) - Kiteto Ndg. Fadhili Didani akimkaribisha mgeni rasmi Mhe. Tumaini Magessa wakati maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katiika kijiji cha mbigiri - kata ya Partimbo wilayani Kiteto.Kulia ni afisa maendeleo ya jamii (W) Ndg. Joseph Mwaleba
Afisa Ustawi wa Jamii (W) Bi. Jacline Barongo Kiteto akisoma risala wakati maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katiika kijiji cha mbigiri - kata ya Partimbo wilayani Kiteto.
Mratibu wa ICHF (W) Kiteto Bi.Rufina Haule akihamasisha wananchi kujiunga na ICHF iliyoboreshwa wakati maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katiika kijiji cha mbigiri - kata ya Partimbo wilayani Kiteto.
Meneja wa Benki ya CRDB - Tawi la Kiteto Bi. Lucia John akiwasilisha mada kuhusu mikopo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katiika kijiji cha Mbigiri - kata ya Partimbo wilayani Kiteto.
.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wilayani Kiteto akiwasilisha mada ya wanawake na maendeleo ya viwanda wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Mbigiri - kata ya Partimbo wilayani Kiteto. .
Mshereheshaji ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bi.Janeth Kawau akitekeleza jukumu lake wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Mbigiri - kata ya Partimbo wilayani Kiteto. .
Wananchi wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa) wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Mbigiri - kata ya Partimbo wilayani Kiteto.
Vikundi mbalimbali vya wanawake vikitoa burudani mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Mbigiri - kata ya Partimbo wilayani Kiteto
.....HABARI KAMILI.....
Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mheshimiwa Tumaini Magessa amewataka wanawake kutumia fursa zilizopo ndani na nje ya wilaya kujikwamua kiuchumi.Mhe. Magessa ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Mbigiri - kata ya Partimbo wilayani Kiteto mapema wiki hii.
Mhe. Magessa amesema kwamba kwa sasa fursa za kiuchumi ni nyingi sana na serikali imekwisha weka mazingira wezeshi ya wanawake kujikwamua . Vilevile Mhe. Magessa amewataka wanawake ambao ni viongozi kuwasaidia wanawake wenzao ili waweze kuinuka kiuchumi. Akisisitiza kuhusu hilo Mhe. Magessa anasema ‘‘ viongozi wanawake katika maeneo mbalimbali ya kijamii na kiuchumi watambueni wadau wenzenu na muone ni namna gani mtawapa usaidizi wenye tija na endelevu ili kuwainua katika nyanja mbalimbali na muwasikilize pale wanapohitaji kufanya jambo fulani la kimaendeleo’’.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi ,afisa ustawi wa jamii (W) Kiteto bi Jacline Barongo amesema kwamba katika kipindi cha Januari hadi Novemba 2017 idara ya maendeleo ya jamii wilaya ya Kiteto imepokea malalamiko 157 , malalamiko ambayo yalihusisha kupigwa mke au mume,kutelekeza familia na kutowapa watoto haki ya kupata elimu.
Naye mratibu wa bima ya afya kwa jamii (ICHF) bi Rufina Haule amewahimiza wanawake kujiunga na ICHF iliyoboreshwa ili wao pamoja na familia zao wawe na afya bora,waweze kufanya shughuli za kiuchumi. Akisisitiza kuhusu umuhimu wa kujiunga na ICHF iliyoboreshwa, bi Haule anasema ‘‘Huwezi ukafanya shughuli yoyote ya kiuchumi kama afya yako ni dhaifu’’ .
Kadhalika bi Haule amesema kwamba ICHF imefanya maboresho makubwa , vipengele kadhaa ambavyo vilikuwa kikwazo kwa wanachama katika kupata baadhi ya huduma za matibabu vimeboreshwa.Bi Haule amevitaja vipengele hivyo ambavyo ni ; Uandaaji na uandikishwaji wanachama.Kupata matibabu , ambapo sasa kwa kutumia kadi ya ICHF mwanachama na wategemezi wake watapata matibabu katika hospitali ya wilaya na rufaa .Awali huduma za bima hiyo zilikuwa ikiishia katika ngazi ya zahanati . Kuongezwa kwa vipimo kama vile X – Ray, utra sound na kumuona daktari (Consultation) ,badala ya vipimo vya malaria na homa ya matumbo ( typhoid) tu vilivyokuwa vikilipiwa awali.
Katika hatua nyingine meneja wa benki ya CRDB tawi la Kiteto bibi Lucia John amewahamasisha wanawake kuchukua mikopo na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili waweze kuinua uchumi wao,ambapo amewataka wanawake walio tayari , kufika katika benki ya CRDB tawi la Kiteto lililopo katika mji mdogo wa Kibaya ili kupata mikopo. Sambamba na hayo bibi John amesema kwamba yeye kwa kuwa ni mwanamke atawapa kipaumbele, kwani anataka wanawake wenzake waweze kujikwamua kiuchumi na kuungana na wanaume katika kuimarisha uchumi wa viwanda.
Siku ya wanawake duniani huadhimishwa Machi 8, kila mwaka,ambapo kwa mwaka 2018 maadhamisho ya siku hiyo yamebeba kauli mbiu isemayo ‘‘Kuelekea uchumi wa viwanda, tuimarishe usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake vijijini’.