Madereva pikipiki na bajaji wilayani Kiteto wameguswa na madhara ya vitendo vya rushwa vinavyotokea kwenye jamii hali ambayo imewapelekea kujiunga kuanzisha Klabu ya Wapinga Rushwa kwa Madereva wa Pikipiki na Bajaji yenye wanachama 35.
Akitoa taarifa kwa Mkimbiza Mwenge wa Kitaifa, Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Ndg. Ismail Habibu, amesema kwamba klabu hiyo imeanzishwa kwa lengo la kukusanya vijana wengi watakaojiunga katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kujengeana uwezo wa ufahamu juu ya maswala ya rushwa.
“Kwakuwa shughuli ya udereva wa pikipiki na bajaji kwa kiasi kikubwa inafanywa na vijana, hivyo tutaweza kukusanya vijana wengi kama wanachama wa klabu yetu na kwa pamoja tutashirikiana na TAKUKURU katika kupambana dhidi ya rushwa”, amesema Mwenyekiti huyo.
Akiongea mara baada ya kupokea taarifa ya klabu hiyo, kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Ndg. Ismail Ali Ussi kampongeza kamanda wa TAKUKURU wilayani hapa kwa kupambana na rushwa. Aidha kiongozi huyu alioneshwa kufurahishwa kuona kwamba TAKUKURU ilianza kupambana na rushwa kwa kuanzisha klabu kwenye shule za msingi, sekondari na sasa kwa madereva wa pikipiki na bajaji.
Aidha kiongozi huyo alitoa wito kwa madereva hao kuhakikisha wanatoa elimu ya kuzuia rushwa kwa abiria wao wote.
Klabu hiyo ambayo imezinduliwa na Mwenge wa Uhuru Julai 13, 2025 ina lenga kutoa elimu kwa wana klabu juu ya umuhimu wao katika mapambano dhidi ya rushwa, kuwahamasisha abiria kutoshiriki vitendo vya rushwa katika Uchaguzi Mkuu 2025 pamoja na kufichua na kudhibiti vitendo vya rushwa wilayani hapa.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa