Madereva wa magari yanayofanya safari za Mbigiri na Matui wamekubaliana na agizo la Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto la kuhakikisha magari yote yanapakia na kushusha abiria katika Stendi Kuu ya Wilaya badala ya kutumia stendi bubu.
Makubaliano hayo yamefikiwa Septemba 25, 2025 katika kikao kilichoongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri, Bi. Irene Mosha, akishirikiana na Mkuu wa Divisheni ya Biashara, Bi. Prisca Mjema.
Akizungumza katika kikao hicho, Bi. Mosha alisisitiza kuwa hatua hiyo inalenga kuboresha mpangilio wa usafiri, kuongeza usalama wa abiria na kukuza mapato ya Halmashauri.
Kwa upande wao, madereva waliridhia kwa kauli moja kutekeleza agizo hilo na kuahidi kushirikiana kuhakikisha agizo hilo linafuatwa.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa