Wilaya ya Kiteto imeadhimisha Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa shughuli mbalimbali za kijamii zilizofanyika Desemba 9, 2024. Katika maadhimisho hayo, viongozi wa wilaya, watumishi wa umma, na wananchi walijitokeza kwa kushiriki katika upandaji wa miti kwa lengo la kulinda mazingira, kufanya usafi katika maeneo ya umma, na kuimarisha mshikamano kupitia bonanza la michezo.
Shughuli hizo zililenga kuhamasisha uzalendo, mshikamano wa kijamii, na uwajibikaji katika kulinda rasilimali za taifa huku zikikumbusha umuhimu wa kushirikiana katika maendeleo ya wilaya na taifa kwa ujumla. Maadhimisho haya yalibeba ujumbe wa "Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananichi ni Msingi wa Maendeleo Yetu"
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa